MAZAZI YA IMAM ALI KUNA SOMO LA KUJIFUNZA-SHEKHE JALALA
Imeelezwa kuwa ikiwa ni kipindi cha takribani karne 14
zimepita toka kutokea kifo cha mwanafunzi wa Mtume Muhammad (Rehma na Amani
ziwe Juu yake), Waislamu na wasio Waislamu wametakiwa kuusoma utawala wa Imam
Ali kwani katika utawala huo kuna mambo mengi ya kujifunza yatakayosaidia
kuwatendea haki wananchi tunaowaoongoza.
Akizungumza na FULLHABARI BLOG katika kumbukizi ya Mazazi ya Imam Ali
ofisini kwake, kiongozi mkuu wa Chuo cha Kiislamu (Hawza) Immam Swadiq Sheikh
Hemed Jalala, alisema kuna somo kubwa la kujifunza katika utawala Imam Ali.
Shekhe Jalala alitaja baadhi ya mambo muhimu ambayo
unaweza kuyapata katika utawala wake ni jinsi ambayo alikuwa akiongoza umma wa
watu huku akimtanguliza Mungu.
Alisema Utawala wa Imam Ali ulitawaliwa na hofu ya Mungu
jambo ambalo lilisaidia kupunguza vitendo vya ufisadi, vitendo vya kuminya haki
za binadamu na watu wengi kuwa na moyo wa kuwajibika.
Alisema Enzi zake, viongozi walikuwa na hofu ya Mungu,
kila mtu alikuwa anafanya kazi kwa moyo wake bila kubagua rangi jinsia na dini
husika.
“Niwape kisa kimoja, Enzi zake Imam Ali wakati akiwa
anatembea tembea akiwa barabarani akamuona mzee akiwa anaombaomba akauliza vipi
huyu; Wasaidi wake wakamwambia yule ni yahudi akasema wakati akiwa na nguvu
zake hamkuyaona hayo sasa, naagiza kuanzia leo mtu huyu awe analipwa mshahara
na serikali”
Kisa hicho kinaonyesha ni jinsi gani asivyokuwa mbaguzi,
na kwamba watawala wanapaswa kutokuwa wabaguzi kama alivyo Imam Ali.
Aufananisha Utawala wa Magufuli na Imam Ali
Katika hatua Nyingine, Sheikh Jalala ambaye pia ni Kiongozi
mkuu wa Waislamu dhehebu la shia Ithnasheria amesema kama linakuja suala la
kufafanisha uongozi basi kwa mbali utawala wa Magufuli unaonekana kufuata nyayo
zake.
Sheikh Hemed Jalala amesema hatua zinazochukuliwa na
Rais Magufuli zinafanana kwa mbali na Imam Ali ambaye mara nyingi alikuwa
anachukizwa na watu kutowajibika katika majukumu yao.
Ukimuangalia Rais Magufuli amekuwa akitumia muda mwingi
kuhakikisha serikali yake inakuwa na watu wachapa kazi, waliokuwa tayari
kuwatumikia watu badala ya matumbo yao.
“Ndugu zangu
nataka nitumie fursa hii kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais John
Magufuli, bila shaka kwa kasi anayoenda nayo taifa litapiga hatua kubwa na
kufanya wananchi wa hali ya chini kunufaika na rasilimali zilizopo”
Alisema Ukimsoma Imam Ali (Mwanafunzi wa Mtume Muhammadi
Rehma na Amani ziwe juu yake) utagundua kuwa katika utawala wake hakupenda
wananchi wa hali ya chini kunyanyasika, na pia alitilia mkazo wa watu wake
kutafuta elimu popote pale.
Amesema jambo hilo pia limeonyesha kwa vitendo na Rais
wa awamu ya Tano Rais John Joseph Pombe Magufuli hususani pale alipotangaza
kuwa Elimu bure hadi kidato cha nne.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni