Zinazobamba

BAADA YA "FACEBOOK, WHATSUPP" KUFANIKIWA, SASA TIGO YAJA NA YOU TUBE YA BURE KUANZIA 6USIKU HADI 12 ASUBUHI


Mkuu wa kitengo cha vifaa na mawasiliano wa Tigo David Zakaria akitangaza kuanza kwa huduma hiyo mpya kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo ambapo sasa wataweza kutazama video Bure ndani ya YouTube kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi na mbili Alfajir.
 Kampuni ya simu ya mkononi nchini Tanzania inayoongoza kwa huduma bora za kidigitali TIGO imetangaza ofa kabambe kwa wateja wake zaidi ya Milioni 10, kwa kuwapatia fursa ya kuangalia video mbalimbali bure kupitia YOU TUBE
 
Tigo Imetangaza huduma hiyo mapema hii leo katika kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika makao makuu ya Kampuni hiyo Makumbusho Jijini Daresalaam
 
Akizungmza na Waandishi wa habari Mkuu wa kitengo cha Vifaa na mawasiliani wa Tigo Bw. David Zacharia amesema hiyo ni kwa mara ya kwanza Kampuni ya simu kutoa ofa ya ukweli kama hiyo.
 
Amesema Wateja watafurahia kusikiliza video mbalimbali ndani ya You tube bure, na zaidi wanauwezo wa kudownload video hizo na kuangalia katika muda wanaoutaka iwe mchana au usiku.


leo imetangaza upatikanaji wa huduma ya bure ya kutiririsha video za youTube nyakati za usiku kwa watumiaji wake wote ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa huduma hiyo kwenye mitandao ya kijamii  bila tozo hapa nchini.

Akizungumzia upatikanaji wa huduma hiyo, David Zakaria amewaeleza wanahabari kuwa huduma ya kutiririsha video za youTube bure itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa tigo kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi na mbili alfajiri ambapo wateja wa Tigo Zaidi ya million kumi watanufaika na huduma hiyo.

Amesema kuwa kitu pekee kinachohitajika ili kuweza kupata huduma hiyo ni kuwa na aina ya simu yenye uwezo wa internent ambapo amezidi kusema kuwa huduma hiyo inazidi kuonyesha wazi jinsi gani mtandao wa Tigo umekuwa ukijituma kwa watumiaji wake ili kuwapa huduma bora Zaidi za kimtandao.
Meneja mawasiliano wa Tigo JOHN WANYANCHA akisisitiza jambo mbele ya wanahabari juu ya Huduma hiyo
Aidha pamoja na utiririshaji huo wa video youTube wateja watakuwa na njia mbadala ya kuweka video kwenye simu zao ambayo ni program ya simu inayojulikana kama youtube Offline inayomwezesha mtumiaji kuongeza video kwenye simu yake ili aweze kuiangalia baadae wakati ambapo muunganisho wa internent unakuwa haupo au upo chini.

Pamoja na hayo kwa video ambazo pale ambapo zinapatikana watumiaji wanaweza kuchagua kuongeza video kwa kuzitiririsha na kwa ajili ya kuangalia hapo baadae kwa kutumia kitufe cha offline ambapo ikiwa imeshachukuliwa kwa njia hiyo video hiyo inaweza kuchezesha bila kuunganishwa na internent kwa muda wa hadi saa 48 hivyo mtumiaji anaweza kuzifurahia video zake za youtube bila hofu ya muunganisho wa internent kuwa yapo chini.

Zakaria ameongeza kuwa kuzifikia data bure kutakuwa kunapatikana kwa wateja wa Tigo malipo kabla bila kuwepo malipo maalum yanayohitajika kuifurahia huduma hiyo.utiririshaji wa video za bure kutoka youTube umefanyika baada ya Mtandao huo kutangaza huduma nyingine za bure ambazo ni whatsapp kwa wateja wake ambapo pia ilitanguliwa na kuzinduliwa kwa huduma ya  Facebook ya kishwahili hapo mwaka 2014.

Mtandao wa YouTube ulizinduliwa mwaka 2005 ambapo unatumiwa na wafuasi Zaidi ya Billion moja duniani kote takribani theluthi moja yake wakiwa wanatumia internent.ambapo imekuwa ikiwapa nafasi wateja wake kutizama video mbalimbali,pamoja na kutoa maoni kuhusu video hizo.

Hakuna maoni