HATIMAYE USAFIRI WA TRENI KUTOKA DAR HADI MWANZA NA KIGOMA WAREJEA,TRL YASEMA HALI IPO SAFI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Afisa Habari wa TRL,Midraji mahezi akizungumza na waandishi wa habari leo,Jijini Dar es SalaaM |
KAMPUNI ya Reli nchini (TRL) imerejesha katika hali
yake usafiri wa Treni ya Deluxe kutoka
Bara hadi Kigoma pamoja na maeneo mengine ya nchi.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Kurejea usafiri huo kutokana na kutengemaa kwa eneo korofi baina ya stesheni
za Kilosa mkoani Mgorogoro na Gulwe Mkoani Dodoma ambapo maeneo hayo yalikuwa
korofi kutokana na mvua zinazonyesha
maeneo hayo na kupelekea kuharibika
miundombinu ya reli.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwaniaba ya Kaimu
mkurugenzi Mtendaji wa TRL Masanja
Kadogosa,Afisa Habari wa TRL Midladjy Maez amesema kwa mujibu wa Taarifa kutoka
kwa wakuu idara za uendeshaji wa Kampuni hiyo
iliyotolewa Aprili 26 mwaka huu
baada ya kufanya ukaguzi wa kina katika eneo la
Gulwe wamejiridhisha kuwa hali imetengemaa.
“Wachunguzi wetu wamesema eneo la Gulwe kwa sasa
linapitika kutokana na kuimalika kwa tuta na kuwezesha treni zote za abiria na
mizigo kupita kwa usalama kabisa”amesema Maez.
Maez ametoa mchanganuo wa safari za Treni pamoja mda wake ambapo Safari
za kawaida kutoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza na Kigoma itaanza siku ya Jumanne Mei 3,2016,huku Treni ya Dulexe
itaondoka Dar es Salaam kila siku ya Jumapili saa 2.00 usiku.
Hata Hivyo,Maez ameleza kuwa Treni ya kutoka Mwanza
na Kigoma kuja Dar es Salaam itatoka huko kila siku ya Alhamisi na Jumapili
kwaanzia mda wa 11.00 jioni na saa 12 jioni kwa Mwanza,huku Treni ya Dulexe
nayo itatoka Kigoma au Mwanza kila siku ya Jumanne saa 2.oo usiku.
Pamoja na hayo,Maez aliwataka wasafiri wote kufanya
utatibu wa Safari mapema (booking) katika stesheni za TRL na sio mahara
pengine.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni