WAZIRI MUHONGO AMJIA JUU ZITTO KABWE,NI KUHUSU KAMPUNI YA IPTL,MZIMU WA ESCROW KURUDI TENA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Waziri wa Nisharti na Madini,Sospeter Muhongo |
NA KAROLI VINSENT
SIKU
chache kupita baada ya Mbunge wa Kigoma mjini,Zitto Kabwe kusema tangu utawala
wa Rais John Magufuli kuingia
madarakani,Kampuni ya kufua umeme ya Independent
Power Tanzania Limited (IPTL)
imeitia hasara serikali ya Bilioni 36 kwa kile anachodai Kampuni hiyo
inaitapeli serikali kwenye Malipo ya
Capacty Charge,
Naye Waziri wa Nisharti na Madini,Sospeter Muhongo
ameibuka na kusema Mbunge huyo anatumiwa kuisakama kampuni ya IPTL kwa maslahi
yake kisiasa,
Waziri Muhongo ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar es
Salaam,wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa Fullhabari.blogs mara
baaada ya kumalizika mkutano na waandishi wa habari aliokuwa anazungumzia
ugunduzi mpya wa Gesi asilia,
Ambapo Waziri Muhongo ni kama amemshangaa mbunge
huyo kwa kitendo chake achodai ni kushikilia hoja ya IPTL kila siku badala ya
kutamaza mikataba yote ya Makampuni ya umeme ambayo inauzia umeme Tanesco ambayo amekili ni
mibovu,
“Yaani huyu mtu anaugomvi tu na hii kampuni na
anaitumia kwa ajili ya kujijenga kisiasa,maana kila siku yeye na IPTL tu,kama
hoja ni mikataba ni mbovu,ni makampuni yote yanayoiuzia shirika la umeme
Tanesco mikataba mingi inakasoro nyingi,lakini nashangaa huyu Zitto ayasema
haya kila siku na IPTL,mbona mengine hasemi”amesema Waziri Muhongo,
Waziri Muhongo ameongeza kuwa “na nyinyi wanahabri
tumieni elimu yenu kuelimisha umma,tuache kuingia kwenye mitego ya wanasiasa wa
aina hii,tusema ukweli juu ya mkataba wa IPTL na Tanesco”
Kauli ya Waziri Muhongo inakuja ikiwa Mbunge huyo ambaye ni Kiongozi wa mkuu wa
Chama cha ACT-Wazalendo kuandika kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo aliandika kuwa kitendo cha
Rais Magufuli kushindwa kuchukua hatua juu ya malipo ya IPTL ambayo yanalipwa
na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kila mwezi yamepelekea sasa hivi kufikia
jumla ya bilioni 36 kupotea,
"Tshs bilioni 8 kila mwezi TANESCO bado
wanalipa IPTL. Rais haijampendeza kumaliza ufisadi huu. IPTL nadhani ni Jipu la
Mgongoni (kwa kutumia maneno ya Hidaya wa Richard Mabala ). Raisq, kwa
kutochukua kwake hatua, ameshaliingizia taifa hasara ya tshs 36 bilioni toka
aingie madarakani" aliandika Zitto Kabwe.
Aidha,Zitto Kabwe aliongeza kusema kuwa Wakati Rais Magufuli
anatimiza siku 100 toka kutangazwa kama Rais Zitto Kabwe alitoa tathimini yake
na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa
ambazo wamelipwa IPTL/PAP kwa siku 100 tu zingeweza kununua CT Scan kwa
hospitali zote za mikoa nchini,
"Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya
Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP
kila mwezi.
"Katika siku 100 tangu Rais Magufuli
aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo
zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni