MCHEZO MCHAFU ZANZIBAR WABAINIKA,CCM NA POLISI WAHUSISHWA,SOMA HAPO KUJUA
Askari wakiwa kwenye meli wakisafirishwa kwenda kisiwani Pemba |
MAANDALIZI ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kushika dola visiwani Zanzibar yanafanywa kwa kutumia
vitisho vya kijeshi, anaandika Mwandishi Wetu.
Mwandishi wa habari hizi aliyepo visiwani humo
anaarifa kwamba, kinachofanywa kwa sasa ni kuzidisha hofu kwa Wazanzibari ili
kupunguza misimamo ya kugomea uchaguzi huo jambo ambalo linatajwa kutoiacha
Zanzibar salama.
Mwandishi huyo aliyepo
Darajani, Zanzibar anaarifu kuwa, tayari wananchi wanaamini kwamba visiwa hivyo
(Pemba na Unguja) vinaweza kuvurugika muda wowote kutokana na matukio
yaliyotangulia pia kuongezwa kwa wanajeshi pamoja na vifaa vyao.
“Yapo mambo ambayo
yanaongeza hofu zaidi, idadi kubwa ya wanajeshi hapa visiwani inaongeza
wasiwasi. Lakini bado kuna kundi la watu ambao wanaonekana kabisa kutoogopa
chochote,” anaarifu mwandishi huyo leo asubuhi na kuongeza;
“Chama cha CUF
hakijatikisika mpaka sasa, taarifa yao ya jana bado inaonesha kuwashibisha
wanachama wake kuendelea kuwa na msimamo kama wa viongozi wao.”
Jana Hamad Masoud
Hamad, Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Umma CUF amethibitisha kuwepo
kwa hofu inayojengwa na Serikali ya CCM visiwani humo akitaja sehemu ya hofu
hiyo kuwa ni kuongezwa kwa wanajeshi huku wengine wakiepelekwa Pemba ambapo
ndio ngome kuu ya CUF.
“Jamani, kwani kuna
nini Pemba mpaka ifikie hali hii au kwa sababu wananchi wameikataa CCM?”
amehoji Hamad na kuongeza kwamba, tayari wananchi visiwani humo wameanza kuhama
makazi yao na kukimbilia njia ya kuelekea Mombasa, Kenya.
Hofu hiyo inajengwa
pia na mauaji yaliyofanywa mwishoni mwa Desemba 2000 chini ya uatwala wa
Benjamin Mkapa ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuzalisha wakimbizi nje ya
nchi kwa sababu za kisiasa.
Jana, viongozi wa dini
walikutana visiwani humo kuzungumzia amani huku wakihimizana kukataa kudumishwa
kwa njia ya mtutu.
Mwandishi wetu
anasema, viongozi wa serikali visiwani humo wamekuwa wakifanyia kazi kwa
ukakamavu kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati alipokutana na wazee wa
CCM Dar es Salaam kwamba, atawashughulikia wale watakaoleta fyokofyoko.
Anaarifu kuwa, hali
ilivyo kwa sasa Zanzibar ina viashiria vyote vya matumizi ya nguvu katika
kuhakikisha kwamba, CCM inaendelea kukalia usukani wa kuongoza kisiwa hicho
licha ya matokeo ya tarehe 25 Oktoba mwaka jana kuonesha kushindwa.
Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC) imetangaza marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya kufuta ule
wa Oktoba mwaka jana kinyume cha katiba.
Kwenye uchaguzi huo
vyama 10 kati ya 14 vimegoma kushiriki lakini ZEC imelazimisha na kuviweka
kwenye orodha ya vyama vitakavyoshiriki.
Habari hii kwanisani ya Mwanahalisi oline
·
Hakuna maoni
Chapisha Maoni