LOWASSA ALEA AMANI YA NCHI,SOMA HAPO KUJUA
Edward Lowassa, aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya Ukawa |
KIMSINGI, kuna tofauti kubwa kati ya binadamu mmoja
na mwingine kwenye mambo mengi. Hii ifahamike hivi, anaandika Adam Mwambapa.
Kama ilivyo kwangu na kwako,
ndivyo ilivyompendeza Mwenyezi Mungu kwamba, binadamu tuwe sawa kwa mwonekano
na maneno au pengine hata matendo; wakati kiundani ni tofauti kabisa.
Ni
ukweli usiopingika nikisema, hata mapacha waliozaliwa siku moja na saa moja,
isipokuwa kwa kupishana sekunde tu. Pia na wao hawako sawasawa kwa kila kitu.
Yule
ni yule na huyu ni huyu. Waingereza wanatumia neno zuri sana, kuwakilisha
utofauti wa kitu kimoja na kingine wakisema ‘unigue’.
Ndilo
neno linaloonesha upekee wa mtu, na ndilo linaloleta tofauti kati ya mtu mmoja
na mwingine. Hata kama kimtazamo wako na mwonekano, vitu viwili utaviona ni
kama viko sawa hivi.
Kwa
Rais Dk. John Magufuli pia na kwa aliyekuwa mshindani wake wa jirani, katika
mbio au kinyang’anyiro cha urais, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Edward
Lowassa; pia wana utofauti mkubwa na hawafanani.
Hata
kama walikuwa na nguvu zinazokaribia kuwa sawa, wote wakitumia maneno ya kuleta
mabadiliko, ingawa Magufuli aliiga, hawako sawa kwa mambomengi.
Lakini
kuna tofauti ya ndani ambayo nguvu na mamlaka yao, kamwe haviwezi kuwa sawa.
Kama nitakavyofafanua.
Kuna
vitu vinajulikana zaidi kwa jina la ‘nafsi’ na kingine kinajulikana kwa jina la
‘nafasi’, asilani vitu hivi havifanani na vina maana tofauti pia. Ingawa,
katika hali ya ubinadamu, wapo wanaovichanganya kwa kuvielezea maana yake iko
sawa na vinafanana. Ukweli havifanani kabisa.
Wakati
tafsiri nzuri ya ‘nafsi’ ni ‘hakika’. Tafsiri ya ‘nafasi’ ni ‘kujaaliwa’ au
‘Iliyojaaliwa/imejaaliwa. Kwa maana hiyo basi, ukiyachanganya, ukisema ‘nafsi
nafasi’ maana yake ni ‘baraka’.
Na
ukisema, ‘nafasi nafsi’ ni ‘neema’. Kwa maana ya kwamba, nafasi inachukua
tafsiri ya neno lingine na kuwa eneo, wakati huo nafsi inaweza kuchukua tafsiri
nyingine inayoweza kueleweka kama mtu.
Pengine
niseme hivi, huenda nitaeleweka vizuri, katika kitu chochote ni lazima kuanze
na vitu hivi viwili.
Ikiwa
ilianza kuweko ‘nafasi’ kabla ya ‘nafsi’ kuwepo, basi nafasi ndicho kitu cha
kwanza na ndipo nafsi hufuata baadaye. Vivyo hivyo, ikiwa kama nafsi ilianza
kuweko mahali, basi nafasi ndiyo huja baada ya nafsi kuwepo.
Ni
wachache sana wasiojua au kuelewa kuwa, kabla ya Dk. Magufuli kuchukua fomu ya
kugombea nafasi ya urais, Lowassa, tayari alikuwa kwenye eneo hilo.
Na
alikuwa amechukua fomu na hivyo akatangulia kuwako na kuwa sehemu ya nafsi
akiisubiri nafasi tu kupata alichokuwa akikihitaji; na baadaye ndipo akaingia
Rais Magufuli kuchukua fomu.
Kilichofuata
wengi wanafahamu fika kwamba, baadaye Lowassa aliingia kwenye mchujo mkali. Au
wa kutopendwa na pengine kuhofiwa, na jina lake likafanyiwa figisu-figisu na
kuondolewa.
Hali
iliyompa nafasi Dk. Magufuli kuwa chaguo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
kuteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya urais, akiwabwaga wagombea
wateuliwa wenzake.
Neema
aliyoipata Dk. Magufuli, ndiyo naizungumzia kama ‘nafasi’ au ‘eneo’ kwa jinsi
nilivyofafanua.
Ukilijua
hilo, nakusihi ulijue na hili. Ni wachache sana mpaka hivi leo wanaoendelea
kuamini wanapoiona amani ikiwa imetawala hapa nchini kiasi cha kutosha, wasijue
imefikaje hapo ilipo na hata kudumu.
Wakati
ilitazamiwa na ilishabashiriwa kuwepo na vita na machafuko mara baada tu ya
uchaguzi mkuu kumalizika na kumpata rais.
Kwa
wasioelewa au kama wanaelewa ila hawataki kuamini, amani hii imeletwa na kitu
kinachoitwa ‘nafsi’. Ile iliyotangulia kuwako kabla ya kuja ‘nafasi’ iliyokuja
baadaye.
Pamoja
na kwamba nilisema kuwa, ‘nafasi’ na ‘nafsi’ havifanani, vinatofautiana na wala
haviko sawa. Ila lazima vitu hivi viwili vishirikiane.
Kama
‘nafasi’ haiitaki ‘nafsi’ ni vigumu hali ya amani kupatikana na kuwepo eneo
husika, muhimu ni kushirikiana na kuelewana kwa ukaribu kutokana na ule umuhimu
wa utendaji wa kila kimojawapo.
Ili
kuwepo au kuleta machafuko hapa nchini. Ni mpaka pale ‘nafsi’ itakapoanza kuona
hakuna haja ya kuwapo na ‘nafasi’.
Au
‘nafasi’ itakapoona hakuna tena haja ya kushirikiana kwa lolote na ‘nafsi’,
katika kuleta maendeleo na ufanisi wa pamoja. Likitokea hili ni hakika vita
itatokea na machafuko kuibuka, jambo ambalo mpaka sasa naamini kuwa limeshikwa
na ‘nafsi’ ambayo ingali inaheshimu uwepo wa ‘nafasi’.
Kwa
tafsiri na maana hiyohiyo, nikimzungumzia Rais Magufuli, nasema kuwa ni mtu
ambaye amepata nafasi ya urais kwa neema, nafasi ambayo haikuwa ya kwake.
Neema
ilianza pale ambapo, yeye binafsi hakuwa na wazo la kuchukua fomu ya kutaka
kugombea nafasi nyeti kama hiyo.
Nafasi
ile, wapo waliotengewa na waliokusudiwa. Kwa ajabu ya wengi, majina yale ambayo
kwa mujibu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja;
yalikuja yakiwa mfukoni mwa kiongozi mmojawapo aliyetaka watu wake wapewe
nafasi.
Jambo
ambalo wajumbe wengi walipingana nalo na lilileta mzozo mkubwa na hatimaye
majina yale kukosa nafasi. Ndipo kwa nasibu, nafasi ikampata na kumwangukia
rais wa sasa.
Kwa
maelezo hayo, baraka za kiuongozi ni lazima na kwa vyovyote, zitaandamana au
zitakuwa na ‘nafsi’.
Na
‘nafasi’ itabaki kuwa na neema tu na kwa kuendeleza utulivu na amani ni mpaka
pale ambapo ‘nafasi’ itaona kuwa ni vyema kutenda au kushirikiana na ‘nafsi’
ili mambo yaweze kwenda na kusonga; nje ya hapo ni mambo kwenda kinyume na
matarajio.
Ieleweke
kuwa amani iliyopo na inayoendelea kuwepo hapa nchini, licha ya kwamba Mungu
ndiye mleta amani na hali ya utulivu, lakini mara zote haji yeye ili watu
tumshuhudie.
Daima
hutumia watu tuliona nao na tunaoishi nao siku zote, na sasa amemtumia Lowassa
kuleta amani kwa ile hali ya kukataa namna yoyote ya maandamano.
Kwa
wale ambao pengine hawakukubaliana na uchaguzi ulivyokuwa na figis-figisu zozote
zilizojitokeza wakati wote wa zoezi lile, pamoja na kwamba inadhaniwa serikali
iliagiza magari mengi ya kivita, yakiwemo mengi ya kubeba maji ya washawasha.
Yote
hayo hayana nafasi kwa wakati huu, maana hali ni shwari.
Makala hii imeandikwa kwenye gazeti la MwanaHALISI la Machi 14-20
mwaka huu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni