PATA STORY KUHUSU KONGAMANO LA TATU LA KISUKARI AFRIKA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani kulia ni Naibu Waziri wa Afya na maendeleo ya Jamii Dk Hamis Kingwangalla akikalibishwa kwenye Kongamano la tatu la wanasansi wa ugonjwa wa kisukari |
KONGAMANO LA TATU LA KISUKARI AFRIKA
EAST AFRICAN DIABETES STUDY
GROUP (EADSG) CONGRESS 2016
Kongamano la tatu la Wanasanyansi wa ugonjwa wa kisukari
limezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Afya Hamis Kigwangala... katika ukumbi wa
Mwalimu Nyerere (JNICC)
Kongamano hilo ambalo litamalizika tarehe 16 March
2016, linaendeshwa na Asasi inayojihusisha na Masuala ya Ugonjwa wa kisukari
Afika Mashariki,asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study
group.
Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha
jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.
Akiongea na waandishi wa Habari, Mratibu wa
Kongamano hilo Doctor Kaushik Ramalya, Kongamano hilo limekaribisha wageni
kutoka nchi nyingine za Afrika ya Mashariki na kusini kushiriki katika
majadiliano na uchunguzi huo wa Kisayansi, ikiwa ni pamoja na kubadilishana
uzoefu wa namana ya kutua matatizo yatokanayo na ugonjwa huo.
Alisema kongamano hilo ambalo linahusisha East
African Diabetes study Group (EADSG) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, litafuatiwa na mkutano Maalum wa
wadau wa kisukari duniani utakaofanyika, Machi 17 hadi 18 2016 katika ukumbi
huo huo wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar Es Salaam,
Tanzania.
Mkutano huo ulioandaliwa na Mfuko wa kusaidia
Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark kwa kushirikiana na Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto nchini Tanzania, pamoja na
Shirika la Afya Duniani Ofisi za Mikoa kwa Afrika pamoja na Shirikisho la
Kisukari duniani utajadili mambo mbali kuhusu namna ya kusaidia wagonjwa wa
ishio na Kisukari kwa kuwa gharama zake ni kubwa mno.
Mikutano hiyo miwili inalenga kutatua tatizo kubwa
la Kisukari linalooendela kukua barani Afrika kwa sasa ambalo limeonekana kukua
mara tatu zaidi ndani ya miaka mitano iliyopita.
Dk. Kaushik alisema kuwa, mbali na mjadala wa
uchunguzi wa kisayansi, Mambo mengine yatakayo jadiliwa ni pamoja na
• Kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari katika nchi
zinazoendelea, na lengo hasa juu Africa na namna ya kutatua matatizo
yatokanayo.
• Kujadili kuhusu mzigo wa kijamii na kiuchumi
unaotokana na watu wenye ugonjwa wa kisukari , familia zao na jamii kwa ujumla.
• Umuhimu wa kutafuta ufumbuzi wa Ugonjwa huu.
• Taarifa za uchunguzi za wataalam ngazi za mkoa.
Aidha utafiti uliotolewa hivi karibuni umeonyesha
kuwa katika kila sekunde sita mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa kisukari (
vifo zaidi ya milioni 5.0 hutokea duniani)
- Mmoja katika watu wazima 11 ana ugonjwa wa
kisukari ( watu milioni 415 duniani kote wanaishina Kisukari)
- Moja katika vizazi saba, huadhirika na ugonjwa wa
kisukari katika kipindi cha ujauzito na kujifungua.
- Robo tatu (75%) ya watu wenye ugonjwa wa kisukari
wanaishi katika nchi chini na kipato cha kati.
- Zaidi ya watu wazima wengi wanakufa kutokana na
ugonjwa wa kisukari kuliko kutokana na VVU / UKIMWI, kifua kikuu na hata
malaria.
- wastani wa milioni 14.2 watu wazima wenye umri
kati ya 20-79 wana ugonjwa wa kisukari katika Kanda ya Afrika.
- Afrika inaongoza kwa wagonjwa wa kisukari ambao
haujatambuliwa, kutokana na kutocheki afya zao; zaidi ya 66.7 % ya watu wenye
ugonjwa wa kisukari hawajui kuwa wana ugonjwa wa kisukari.
- Mtu na kisukari aina ya 2 (Type 2 Diabetes)
anaweza kuishi kwa miaka kadhaa bila kuonyesha dalili yoyote, madhara
yanayoweza kujitokeza ni pamoja na ugonjwa wa figo , moyo kushindwa kufanya
kazi, ugonjwa wa jicho na kusababisha upofu na matatizo ya mguu na kusababisha
ulema.
- Mataifa ya Afrika kwa idadi kubwa ya watu wenye
ugonjwa wa kisukari ni pamoja na Afrika Kusini (2.3 milioni ), Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (1.8 milioni ) , Nigeria ( milioni 1.6 ) na Ethiopia (1.3
milioni).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni