KAMATI YA BUNGE YAITAKA SERIKALI KUWAJENGEA NYUMBA MABALOZI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi na Usalama,Balozi Adadi Rajabu akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kikao cha Kamati yake, |
NA KAROLI VINSENT
MWENYEKITI wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya
Nje na Ulinzi na Usalama,Balozi Adadi Rajabu ameitaka serikali kuanza utaratibu
wa kuwajengea nyumba za kuishi Mabalozi
wetu walioko nje ya nchi ili kuweza kuikoa serikali isipateze fedha,
Hata hivyo,Balozi Rajabu ameishauri serikali
kuharakishia katika kufungua ofisi za Balozi kwenye nchi ambazo zimekuwa na
wakilishi wao hapa nchini,
Akizungumza na Waandishi mara baada ya kumalizika
Kikao chake cha Kamati hiyo ,Balozi Rajabu ambaye ni Mbunge wa Muheza amesema
kwa sasa kamati yake imebaini kumekuwa na upotevu wa fedha nyingi za serikali
kwenye Ofisi za Balozi mbali mbali kutokana kitendo cha serikali kuwakodishia
nyumba za kuishi mabalozi,
Amesema Serikali ingechukua hatua ya kuwajengea Nyumba
Mabalozi wetu katika nchi husika ingechangia kuokoa fedha zinazopotea kutokana
na kuwakodishia nyumba mabalozi,
Kuhusu nchi ambazo hazina Ubalozi wa Tanzania,Balozi
Rajabu ameitaka serikali kuharakisha haraka zoezi ya kufungua ofisi za balozi
katia nchi husika ili kuwasaidia wananchi ambao watahitaji huduma,
“Serikali inatakiwa kufungua haraka Balozi katika
nchi zisizo na Ofisi zetu,kwani Kamati yangu imeona katika nchi ya Korea Kusini
ambayo imekuwa na wawakilishi wengi lakini mpaka sasa haina ofisi ya Ubalozi,”amesem
Balozi Rajabu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni