Zinazobamba

KAMPUNI YA JUMBO CAMERA HOUSE LAJA NA DUKA LA VIFAA BORA VYA PRODUCTION,SOMA HAPO KUJUA




 Kamera za kisasa kibisa zilizopo katika Duka Jumbo



 Bidhaa za production zikiwa ndani ya Duka hilo ambazo ni za kisasa kabisa
 Taa mbali mbali za kutumika wakati kushooting video pamoja na kuwepo kwenye studio za Tewlevisheni


NA KAROLI VINSENT
KATIKA kuhakikisha wanainua sekta ya mbali mbali ambazo  zinatumia Kamera  katika kuleta maendeleo ikiwemo katika kuzarisha vipindi mbali mbali vya Televisheni na pamoja na kazi za Filamu nchini, ambapo Kampuni Jumbo Camera House imezindua Duka la Kisasa la Vifaa hivyo,

Duka hilo ambalo lipo Jengo la Benjamini Mkapa Pension Towers Posta  Mpya,Jijini Das es Salaam,ambapo Duka hilo limesheheni vifaa vya kisasa na mitambo ya vyombo vya habari vya kisasa ambapo hapo awali vilikuwa havipatikani hapa nchini,

Akieleza Ubora wa Vifaa hivyo,Mkuu wa Mauzo wa Jumbo Camera,Mathias Luoga wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Hapa, , amesema Kampuni hiyo ni ya Kitanzania ambayo imedhamilia kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha uhuru wa vyombo vya Habari nchini pamoja na kuwainua wasanii wa kitanzania,

Amesema kuwa katika kipindi cha utandawazi ni kipindi anachodai kuwa  Dunia imekuwa kijiji basi jamii haina budi kuwa na vifaa vya kisisasa vitakavyokwenda sambamba na mabadiliko hayo ya Dunia,


Luoga amezitaja Vifaa hivyo vya Kisasa vinavyopatikana katika Duka hilo  ambavyo amevitaja kuwa ni vya ubora wa juu kuwa ni  Kamera za Chopa, “Drones”,Boom Microphones,Bomm srick,CranesmReli,Winch za Kamera,Slider,Mabegi ya Kamera za aina zote,Masanduku ya kuhifadhikamera wakati wakwenda mbali mbali na Ofisi,
Vifaa vengine vya kisasa vilivyopo Dukani hapo ni Mashine za kichanganyia picha (Video Mixer),Camera monitor,audio recorder,camera cage,Taa mbali mbali za video pamoja na Taa za kuchanganyia picha ,
Hata hivyo Luoga amesema Mbali na kuuza vifaa hivyo vya kisasa pia Duka hilo litakuwa na mpango maalum wa kuwasaidia  wadau kwa kuwaunganisha wataalum wa kuandika michanganuo ya uanzishaji wa studio za Picha mnato na studio za Televisheni.
Luoga amewataka Watanzania kuchangamkia Fursa hiyo kwa kwenda kupata huduma bora za vifaa vya kisasa vinavyopatikana katika Duka hilo,

Maoni 2

Unknown alisema ...

Its a good thing jumbo has brought an opportunity to youths and society at large.my advice please start up a website where you put all tje details of your products plus the costs.by doin so we all get the details and attracted to purchase in that way.

Unknown alisema ...

Its a good thing jumbo has brought an opportunity to youths and society at large.my advice please start up a website where you put all tje details of your products plus the costs.by doin so we all get the details and attracted to purchase in that way.