HATIMAYE SUKARI YASHUKA BEI RASMI,NI AGIZO LA MAGUFULI,BODI YA SUKARI YAWATANGAZIA KIAMA WENYE MADUKA YATAKA BEI ELEKEZWA IWE HII HAPA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa mkuu wa Bodi ya Sukari nchini,Henry Semwaza akizungumza na Waandishi wa Habari(Hawapo pichani) mda huu Jijini Dar es Salaam,
NA KAROLI VINSENT
HATIMAYE
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imekisikia kilio cha Wananchi kwa muda mrefu
ambao walikuwa wakilalamikia bei juu ya sukari,
Ambapo Serikali hiyo imeibuka na kutangaza bei elekezi ya
SH 1800/ kwa kilo moja Sukari kwenye maduka yote ya rejareja nchini Toka Bei ya Sh 2500 kwa kilo moja iliyokuwa sasa ,
Hata hivyo Serikali imesema haitasita kuwachukulia hatua
kali kwa wauzaji ambao watakikaidi agizo hilo la bei elekezi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mda huu jijini
Dar es Salaam Mkurugenzi wa mkuu wa Bodi ya Sukari nchini,Henry Semwaza amesema Bei hiyo itakakiwa kuanza kutumika mala moja kwenye maduka yote nchini
kwa madai kuwa sahivi hakuna uhaba wa
sukari kwenye Maghala ya kuhifadhia sukari.
Semwaza amesema Wafanyabiashara wote wanapaswa
kuzingatia agizo hilo pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa
na kuuzwa kwa wananchi bila kuhodhi
,
Amebainisha kuwa Maafisa wa Bodi hiyo kwa
kushirikiana na Mamlaka zengine za serikali kote nchini,hususani Maafisa wa
Biashara wa mkoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa Agizo hilo
,
Amesisitiza kuwa Bodi hiyo haito shindwa kuchukua
hatua stahiki za kisheria kwa wale wataobainika kupandisha bei au kuhodhi
bidhaa hiyo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni