Zinazobamba

HALI YA MAUZO KATIKA SOKO LA HISA KWA HII,NI HII HAPA,BOFYA HAPO KUJUA



 
Meneja Masoko wa DSE Patrick Mususa wakati wa mkutano na waandishi wa Habari akielezea hali ya mauzo katika soko la hisa

Mauzo ya soko
Idadi ya mauzo imepungua kwa 53% hadi Bilioni 2.5 kutoka  Billionin 6.3 
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imepungua [Patrick Mususa] hadi 4.6 kutoka milioni 6.6.

Kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     CRDB kwa asilimia 96%
2.     TBL kwa asilimia 1%
3.    TOL kwa asilimia 1%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umebaki kwenye kiwango kile kile cha trilioni 21 wiki hadi wiki.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha trilioni 9 wiki hadi wiki.

Mabadiliko ya bei za hisa
Kampuni tatu zimeongoza katika ongezeko la bei ya Hisa zikiwa ni:
1.       KCB kwa ongezeko la bei la asilimia 5%
2.       ACACIA kwa ongezeko la bei la asimilia 4%
3.       NMG kwa ongezeko la bei la asilimia 2%
Viashiria (Indeces)
·      Kiashiria cha sekta ya viwanda kimeshuka kwa pointi 70.27 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta ya (3.88 %)TCCL, (2.36%) TPCC na (1.97%)TBL .
·      Kiashiria cha sekta ya huduma za kibenki na za kifedha kimeshuka kwa pointi 74.66 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta ya NMB bank kwa asilimia 4.48%% na CRDB kwa 1.25%.
·      Kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara kimepanda kwa pointi 20.93 kikiwa kimechangiwa na ongezeko la bei ya hisa za SWISSPORT kwa asilimia 0.72%.


Usajili wa shindano la wanafunzi
Usajili wa wa shindano la wanafunzi wa vyuo vikuu umeanza, tunatoa wito kwa wanafunzi wote washiriki kwenye kujisali kwa kupitia application ya leverage inayopatika kwenye Playstore na App store. Vile vile wanaweza kwenda kwenye tovuti ya shindano www.younginvestors.co.tz na kujisajili humo.
Hadi sasa wanafunzi 130 wa vyuo vikuu mbali mbali vya Tanzania wameshajisajili katika shindano.

Hakuna maoni