ZITTO KABWE AWA MBOGO UFISADI WA BENKI YA STANBIC,AISHIKA PABAYA SERIKALI YA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo)
ameitaka serikali kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ili
kubaini wizi wa Sh. 608 trilioni zilizokopwa kupitia Benki ya Stanbic yenye
tawi lake nchini hapa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma …
(endelea).
Ametoa kauli hiyo leo bungeni
wakati akiuliza swali la nyongeza kutaka kujua ni hatua gani ambazo
zinachukuliwa kutokana na ufisadi mkubwa wa fedha hizo ambazo ni trilioni 6.8.
“Jumla
ya fedha ambazo serikali ilizikopa nje kwa mfumo wa namna hiyo ni shilingi
trilioni 6.8 na katika taarifa ya hukumu inaonesha mtindo huo wa kutumia
vikampuni kwa ajili ya kupata mikopo imekuwa ikitumika na mabenki mengi ya
kibiashara hapa nchini.
“Serikali
haioni kwamba umefika wakati CAG aweze kufanya ukaguzi maalum wa mikopo yote ya
kibiashara ambayo serikali imechukua katika kipindi hicho ili kuweza kujua kama
pia kulikuwa kuna aina za rushwa za namna hiyo ambazo zimekuwa
zinafanyika,”amehoji Zitto.
Zitto
amesema DFA (Hukumu ya Uingereza) ilikuwa ina lengo la kuilinda Benk ya
Uingereza ambayo ndiyo ilitoa hongo kwa maofisa wa Tanzania ili iweze kupata
biashara ambapo alihoji, serikali haioni kwamba ni wakati muafaka sasa kufungua
kesi dhidi ya benki hiyo ya Uingereza ili iwe fundisho kwa kampuni za nje
zinazohonga kwa lengo la kupata biashara katika nchi za kiafrika
Akijibu
maswali hayo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju amesema CAG anayo
majukumu ya kikatiba na hilo ni jukumu ambalo anaweza kulitekeleza wakati
wowote ili kujiridhisha kama mikopo hiyo ambayo imekuwa ikipatikana kwa namna
ambayo inaifanya nchi iingie kwenye hasara.
Amesema,
kama Zitto anazo taarifa zozote zinazoweza kuisaidia serikali ama kufungua
shauti la madai ama jinai ashirikiane na vyombo husika ikiwemo Ofisi ya AG na
kuliangalia ili kuona kama linakidhi sifa na sheria na kwa kuzingatia pia
uhusiano uliopo kwa nchi ya Uingereza ili kuona kama kesi ya jinai inaweza
kufunguliwa.
Aidha
amesema serikali imepokea ushauri wa Zitto na itaufanyia kazi kwa kuzingatia
sheria za ndani ya nchi na uhusiano wa kisheria katika Jumuiya ya Kimataifa.
Awali
katika swali la msingi la Zitto alitaka kujua serikali inaichukulia hatua gani
Stanbic Bank ili walipe fidia zaidi.
“Mwaka
2013 serikali ilizuia hatifungani ya thamani ya dola za Kimarekani milioni 600
(USD 600.0 mili) kupitia Benki ya Sdandard yenye tawi hapa nchini (Stabic).
“Shirika
la Corrupition Watch la Uingereza kwa kutumia vyombo kama IFM imeonesha kuwa
hatifungani hiyo imeipa Serikali ya Tanziania hasara ya Dola za Marekani
miliono 80 na serikali imelipwa fidia Dola za Marekani milioni 6.
“Je
kwa nini serikali haichukulii hatua Stanbic Bank ili ilipe fidia zaidi?”amehoji
Zitto.
Akijibu
swali hilo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashantu Kijaju amesema,
serikali imefuatilia taarifa za hasara kwa Serikali ya Tanzania ya Dola za
Marekani 80 iliyotajwa na Zitto lakini haikupata ushahidi wake.
Hata
hivyo Dk. Kijaju amesema Benki Kuu ya Tanzania imeiandikia Benki ya Stanbic barua
ya kusudio la kuitoza faini ya Sh. 3 bilioni kwa kosa la kufanya miamala
inayokiuka sheria na kanuni za mabenk na taasisi za fedha.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni