WATUMIAJI WA SHISHA HATARINI,KUPATA UGONJWA HUU HAPA,SOMA HAPO KUJUA
WATUMIAJI wa kilevi aina ya “Shisha” wakao hatarini
kupata ugonjwa wa satani zaidi kuriko
wavutaji wa sigara.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa Chama cha Kudhibiti matumizi ya Tumbaku nchini,(UICC)RutiGadi
Kagaruki wakati wa seminina kwa wanahabari iliyoandaliwa na shirikisho la vyama
vya magonjwa yasiyo ya
kuambukiza(TANCDA) ili kuwajengea uwezo wa kujua magonjwa ya yatokanayo na
saratani,
Ambapo Bi
Kagaruki amesema kwa sasa hapa nchini kumekuwa na watumiaji wengi wa kilevi cha
Shisha huku Tafiti zikionyesha watumiaji wengi wa kilevi hicho ni vijana ambapo
watazamiwa kupatwa ugonjwa wa saratani kuriko watumiaji wa Sigara.
“Matumizi ya Shisha yameonekana kwa sasa ni hatari
sana kwani licha ya kuwa na tumbaku nyingi sana lakini watoaji shisha hizo
wamekuwa wakichanganya aina flani ya madawa ili kupunguza harufu ya
tumbaku,lakini licha ya kufanya hivyo ndio wamekuwa wakiweka madawa ambayo ni
hatari zaidi kwa binadamu”amesema Bi Kagaruki.
Bi Kagaruki amesema katika sehemu za starehe
kumekuwa na mwamko kwa vijana wamekuwa wakitumia kilevi hicho kwa kasi huku
akitahadharisha serikali ni wakati wa kuvizuia vilevi hicho kwa hatari la
kuliokoa taifa.
Hata hivyo,Bi Kagaruki amesema Tumbaku huua wavutaji
milioni sita kwa mwaka duniani huku wengine wasiovuta laki sita hufa kutokana na kuvuta moshi huo wa tumbaku.
Amebainisha kuwa matumizi ya tumbaku ni sababishi
kubwa la saratani na vifo vinavyotokana
na saratani na pia magonjwa mengine yasioambukiza,kama moyo,magonjwa sugu ya
kifua na kisukari.
Bi Kagaruki ameongeza kwa kusema kuwa utafiti mdogo
uliofanywa na mwaka 2009 kwenye Taasisi ya saratani ya Ocean Road na Hospitali
ya Taifa Muhimbili ulionyesha kuwa asilimia 32% ya saratani zote hapa nchi
husababishwa na matumizi ya tumbaku.
Hata hivyo Bi Kagaruki ameitaka serikali kurekebisha
sera ya kodi za tumbaku kwa kuzidisha
kodi katika bidhaa zote zitokanazo za tumbako jambo analodai litachangia
kupunguza matumizi ya tumbaku.
Vilevile Bi Kagaruki
ametoa wito kwa wananchi kuacha kutumia matumizi ya sigara,kupunguza ulaji wa nyama nyekundu na
zilizosindikwa,kufanya mazoezi mara kwa mara na kuacha kunywa pompe jambo
analodai linaweza kuongeza ubora wa afya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni