MBUNGE KUBENEA AWACHACHAFYA WABUNGE WA CCM,SOMA HAPO KUJUA
Saed Kubenea, Mbunge wa jimbo la Ubungo |
SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo amelieleza Bunge
kwamba Serikali ya Tanzania inaendeshwa kidikteta. Anaandika Dany Tibason.
Kauli hiyo ameitoa jana bungeni
wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Mwaka Mmoja na kuongeza, serikali
inakamata na kutesa pia hata kuua raia wake na kwamba, usalama wa raia nchini
ni kitendawili.
Kubenea
amesema, serikali pamoja na kujigamba kuwa upo usalama katika suala la ulinzi
lakini imekuwa ikitumika kuwaua raia wake huku watuhumiwa wakishindwa
kuchukuliwa hatua yoyote.
Katika
mjadala huo ambao wabunge wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa wakiomba
miongozi pia taarifa, Kubenea alitaja majina ya baadhi ya raia waliotesa wakiwa
mikononi mwa serikali.
Alimtaja
Daudi Mwangosi ambaye alikuwa mwadishi wa Kituo cha Televishen cha Channel Ten
pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) ambaye
aliuawa akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi Septemba 2012.
Wengine
waliotajwa kama mfano wa ubabe wa serikali katika kutesa raia wake ni pamoja na
Dk Steven Ulimboka ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania
Desemba 2012.
Absalom
Kibanda ambaye amemamilaza muda wake hivi karibuni kama Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri (TEF), alivamiwa Machi 2013 na kujeruhiwa vibaya huku yeye mwenyewe
(Kubenea) akiwa miongoni mwa walioshambuliwa mwaka , mpaka sasa hakuna chochote
kinachoendelea kutokana na mashambulizi hayo.
Hali
hiyo imemsukuma Kubenea kusema kuwa “Tanzania bado haijakuwa na usalama wa
kweli kwa raia wake na ndiyo maana wananchi wanapigwa, wananyanyaswa na kupigwa
huku serikali ikiendelea kufumbia macho jambo hilo.”
Akizungumzia
kuhusu masuala ya Zanzibar amesema kinachoendelea visiwani humo ni ubabe wa
watawala licha ya kuwa serikali iliyopo madarakani kujinadi kuwa ni ya
kidemokrasia.
Kuhusu
uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow Kubenea amesema ni aibu kwa
serikali ya sasa ambayo imeonekana kumrudisha Waziri Sospiter Muhongo ambaye
alifukuzwa na bunge kwa kashfa hiyo.
Amesema,
tume iliyoundwa na bunge na kusababisha mawaziri, wenyeviti wa kamati kujiuzuru
imepuuzwa kutokana na wote ambao walituhumiwa kupata nafasi mbalimbali ndani ya
serikali akiwemo Andrew Chenge.
Amesema
Prof. Muhongo ambaye alifukuzwa na Bunge, ameteuliwa tena kushika wadhifa ule
ule aliotuhumiwa nao, na kwa sasa aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ndiye
mwenyekiti wa Bunge la 11.
Kauli
ya Kubenea ilionekana kuwachoma baadhi ya wabunge hususan CCM ambao mara kwa
mara walikuwa wakitaka mwongozo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni