Zinazobamba

RAIS MAGUFULI AANDAMWA KILA KONA,NI KUHUSU MGOGORO WA ZANZIBAR,SOMA HAPO KUJUA

Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

TUHUMA zimeendelea kuelekezwa kwa Rais John Magufuli kutokana na hatua yake ya kukwepa jukumu la kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar, anaandika Faki Sosi.
Peter Lijualikali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero (Chadema) amesema, hatua yake ya kuupa mgongo mgogoro huo inaashiria kuitenga Zanzibar.
Akizungumza na Mwanahalisi Online leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa kwenye uzinduzi wa programu ya kuwezesha umulikishaji Ardhi, amesema kuwa, hatua hiyo ni ‘utoto wa kisiasa’ na kwamba, yeye kama Raia wa Jamhuri ya Muungano hawezi kuepuka mgogoro huo.
Akiwa kwenye Mkutano na Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam wiki iliyopita, Rais Magufuli alisema kwamba, hatoingilia mgogoro huo kwa madai unapaswa kutatuliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (NEC).
Kauli yake imepingwa na kada mbalimbali nchini zikidai kuwa, anachokifanya rais huyo ni kukimbia majukumu yake sambamba na kutaka kukiokoa chama chake (CCM) kilichoshindwa kwenye uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.
Lijualikali amesema, kauli hiyo inaashiria uvunjifu wa Muungano kutokana na kuyatenga masuala ambayo angeweza kuwajibika kama amiri jeshi mkuu

Maoni 1

Bila jina alisema ...

Huyo raisi anaonesha mpema kuwa anakitazama chama chake na wala hana hajaa
kutenda haki. Ni wazi anaunga mkonomoja kwa moja dhulma zinazotokea Zanzibar na kuwyapeleka majeshi yake huko kufanikisha dhulma hizo. Kweli huyu raisiataendesha na kuzikingia kifuwa dhulma hio kweupe bila ya kujificha. Huko Uganda hata Museveni akichukuwa serikali kwa nguvu, hali yake itakuwa afadhali kuliko yaMagufuli kwababu Museveni kayaanza mambo mapema na kinyume na Zanzibar kwa kuwa huo visiwani matoeo yalikuwa yameshatolewa na washindi kupewa shahada za ushindi jambo ambalo limeshuhudiwa na kutambuliwa duniani kote.