BREAKING NEWS,CUF YATANGAZA MAANDAMANO MAKUBWA DAR,UBABE BABE WA ZANZIBAR WATAJWA,SOMA HAPO KUJUA
Jumuiya ya wanawake wa chama cha wananchi CUF maarufu kama JUKECUF wametangaza kufanya maandamano ya Amani siku ya tarehe 22,mwezi huu wa pili Jijini Dar es salaam yenye adhma ya kupinga hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.
Akizungumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mh severena mwijage amewaambia wanahabari kuwa maandamano hayo yataanzia ofisi kuu za CUF buguruni kuelekea ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh SAMIA SULUHU
Amesema kuwa jumuiya hiyo inatambua kwamba hali ya Amani iliyopo Zanzibar ikivurugika kwa kiasi kikubwa watakaoathirika ni kina mama na watoto hivyo wameona ni bora kufikisha kilo chao hicho kwa makamu wa Rais ambaye ni Mwanamke mwenzao awasaidie.
Maandamano hayo yatapita barabara ya uhuru,ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam,karume,kariakoo,mnazi mmoja,Central polisi,barabara ya sokoine ,Bandarini,mahakama kuu,mahakama ya ardhi,Hadi ofisi ya makamu wa Rais.
Maandamano hayo bado hayajaruhusiwa na polisi licha ya polisi kupata marua kutoka CUF.
Maoni 1
Hawatotowa ruhusa kwasababu woga wanaiogopa haki
Chapisha Maoni