BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE,TAARIFA KAMILI KUHUSU TAKWIMU,SHULE BORA NA WANAFUNZI BORA SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Katibu mtendaji wa (NECTA) Dkt Charles Msonde |
NA KAROLI VINSENT
BARAZA la Mitihani nchini (NECTA) limetangaza
matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2015 ambapo jumla watahiniwa 448,382 waliofanya
mtihani huo ambapo jumla ya
watahiniwa 272,947 sawa na asilimia
67.53 ndio wamefaulu mtihani huo, mbapo kati
yao wasichana ni 131,910 sawa na asilimia 64.84 na wavulana ni 141,034 sawa na asilimia 71.09,
Hata hivyo Jumla ya watahiniwa 94,941 sawa na
asilimia 24.73 ndio waliopata madaraja ya 1 hadi la 111 ambapo kati yao
wasichana ni 38,338 sawa na asilimia 19.63 na wavulana 56,603 sawa na asilimia
29.99,
Vilevile NECTA limetangaza pia kurudisha mfumo wa mwanzo
wa division kwenye upangaji wa matokeo hayo na kuachana na mfumo wa GPA.
Ambapo pia Tasmini ya matokeo hayo imeonyesha
kiwango cha kufahulu kimeshuka kwa asilimia 1.85 kutoka asilimia 69.76 mwaka
2014 hadi asilimia 67.91 mwaka 2015.
Hayo yametangazwa leo Jijini dar salaam na Katibu
mtendaji wa (NECTA) Dkt Charles Msonde Wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Jumla
ya wanatahiniwa 448,389 walifanya
mtihani huo,kati yao wasichana wakiwa ni
229,141 sawa na silimia 51 na wavulana 219,238 sawa na asilimia 48.90,
Sanjari na hao watahiniwa wa kujitegemewa waliofanya
mtihani huo walikuwa 54,417
Dkt Msonde amesema watahiniwa wa shule waliofaulu ni
240996 sawa na asilimia 67 ya waliofanya
mtihani huo, kati yao wavulana walikuwa 124,871 sawa na asilimia 71.09 huku
wasichana walikuwa 116,125 sawa na asilimia 64.84.
Dkt Msonde amesema watahiniwa wa kujitegeme
waliofaulu mtihani huo ni 31,951 sawa na asilimia 64.80 huku watahiniwa wa
mtihani wa maarifa yaani (QT) waliofaulu ni 7,536 sawa na asilimia 46.59
wamefaulu mtihani huo.
Dkt Msonde amesema masomo waliofanya vizuri
watahiniwa ni Civics,Historiya,Geografia,Kiswahili,kingeleza,Kemia
Biolojia,Commerce na Bokk-kiping umepanda kwa asilimia 1.09 ukulinganisha na
mwaka uliopita,
Sanjari na hayo pia Dkt Msonde amezitaja Shule
zilizofanya vizuri (1)Kaizegere mkoani
Kagera,(2)Alliance Girls iliyopo mkoani Mwanza,(3)St Francis Girls iliyopo mkoani Mbeya,(4)
Alliance Boy (5)Canossa iliyopo mkoani Dar es Salaam,(6)Marian Boys mkoani
Pwani,(7)Alliance Rock Army iliyoko
Mwanza ,(8)Feza Girls iliyoko Jijini dare
s Salaam, (9)Feaza Boys iliyoko Jijini dare s Salaam ,(10) Uru Seminary iliyopo Kilimanjaro,
Dkt Msonde pia alizitaja shule kumi za mwisho
kitaifa ambazo ni (1) Shule ya Pande iliyoko mkoa wa Lindi (2) Igawa kutoka
mkoa wa Mogorogo (3) Korona kutoka mkoa wa morogoro (4) Sofi kutoka mkoa wa
Mogorogo (5) Karui kutoka mkoa wa Pwani.
Zengine ni Shule (6) Patema kutoka shule ya Tanga, (7)
Saviak kutoka mkoa wa Dar es Salaam ,(8)Gubali kutoka mkoa
Dodoma (9)Kichangani kutoka mkoa wa Morogoro (10) Malinyi kutoka mkoa wa
malinyi.
Hata Hivyo Dkt Msonde wanafunzi kumi bora kitaifa ambao
ni (1)Butogwa Shija kutoka shule ya Canossa iliyoko jijini Dar es Salaam, (2)
Cogcong Wang kutoka shule Feza Girls iliyoko Jijini Dar es Salaam,(3) Innocent
Lawrence Feza Boys kutoka Jijini dare s Salaam,
Wengine ni (4)
Dominick Aidano kutoka shule ya Msolwa
iliyopo mkoani morogoro (5) Sang’udi Sang’udi kutoka Shule Ilburu kutoka mkoani
Arusha, (6) Asteria Chilambo kutoka mkoani
Dar es Salaam,(7) Belinda Magere kutoka shule ya Canossa mkoani Dar es
Salaam,
Pia (8)
Hufrey Kimanya Msolwa kutoka mkoani Mogorogoro (9) Bright Mwang’onda kutoka
shule Marian Boys Pwani (10) Erick Mwang’ingo
kutoka shule Mariam Boys iliyopo moani Pwani,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni