BENK M YAJA NA KITU BORA KABISA KWA WATEJA WAKE,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Afisa Mtendaji wa Bank M, Bi Jacqueline Woiso akiongea nawaandishi wa habari Pamoja naye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Allan Msalilwa |
NA KAROLI VINSENT
BAADA ya Benki Kuu ya Tanzania kuboresha huduma ya
malipo kwa njia ya hundi, benki M imekuja na mfumo utakaopunguza foleni
katika benki barani Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa bank hiyo Jacqueline Woiso amesema huduma hiyo ya Money.Moja kwa moja itasaidia kupunguza msongamano.
“Wateja wataepuka foleni za barabarani na hawatakuwa na muda wa kukimbizana kuwahi bank kabla hazijafungwa”amesema Woiso.
Amesema kuwa wateja wanaweza kufanya miamala ya hundi wakati wowote na muda wowote kwani mashine hizo wamezisambaza kwa wahusika wake.
“Money.Moja kwa moja ni huduma yenye usalama zaidi inayotumia mtandao wa intaneti ambapo mteja ataweka hundi kwenye kifaamaalum na taswira ya hundu na kutuma moja kwa moja bank”amesema Woiso.
Alisema kwa kufanya hivyo fedha hizo zitaingizwa kwenye akaunti zao bila wasiwasi wowote
Hakuna maoni
Chapisha Maoni