OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YASEMA BEI YA BIDHAA YAPUNGUA,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za
Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko
wa bei mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei
na Ajira Bi. Ruth Minja.
|
MATUMIZI ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua
hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/2012 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kutokana na hali hiyo kunaashiria kupungua kwa umasikini wa kipato kwenye kaya kwa kuelekeza matumizi mengine bidhaa zisizo za vyakula kama usafiri, mawasiliano, makazi, maji pamoja na nishati.
Amesema matokeo yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/2012 kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007.
Amesema kumekuwa na ongezeko la zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye kundi la Mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya mwaka 2007.
Nae Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth Minja amesema baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata Fahirisi za bei zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa ni pamoja na mizania katika bidhaa za huduma muhimu ikiwemo Vyakula, afya, Usafiri, Maji na Nishati.
A

Hakuna maoni
Chapisha Maoni