MEYA WA UKAWA ILALA KUULA MAMILIONI,SOMA HAPO KUJUA
Charles Kuyeko, Meya wa Manispaa ya Ilala (aliyesimama) akiongoza baraza la Madiwani la Ilala |
CHARLES Kuyeko,
Meya wa Manispaa ya Ilala anasubiri kuvuna zaidi ya Sh. 20 milioni ikiwa ni
fidia baada ya kushinda kesi iliyofunguliwa na mpinzani wake Sabir Malilo, anaandika Happyness Lidwino.
Ni baada ya Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini
Dar es Salaam jana kumpa ushindi katika kesi yake ya kikatiba ya kupinga
matokeo ya udiwani iliyofunguliwa na mpinzani wake Malilo.
Uchaguzi uliompa ushindi Kuyeko ni ule uliofanyika tarehe 25
Oktoba mwaka jana kwenye Kata ya Bonyokwa-Tabata, Dar es Salaam.
Malilo alisimama kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku
Kuyeko akikiwakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kuyeko amesema, pesa hizo zinahusu gharama za mawakili wake
wawili waliosimamia kesi yake ambao na kuwa, zipo gharama zingine ikiwemo
usafiri wa yeye na familia yake kwenda mahakamani, chakula pamoja na muda
aliopoteza kufuatilia kesi hiyo na kwamba, anatarajia kupeleka hesabu kamili
mahakamani baada ya kukutana na mawakili wake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Kuyeko amesema, mahakama
hiyo iliifuta kesi ya kikatiba iliyokuwa imefunguliwa na Malilo ikiwa ni baada
ya kujiridhisha na utetezi wake ambapo ilibainika kutokuwepo kwa mashiko.
Amesema, uamuzi wa kufutwa kwa kesi hiyo ulitolewa na Cyprian
Mkeha ambaye ni Hakimu Mkazi Mfawidhi na kuwa, mahakama imeamua kufuta kesi
hiyo baada ya kupata utetezi wa upande wa mshitakiwa uliotolewa na Wakili John
Malya na kutosheleza.
Kuyeko amesema, katika kesi hiyo namba 23 ya mwaka 2015 mlalamikaji
ambaye ni Malilo alipinga matokeo ya ushindi wake kwa madai ya kumwibia kura
katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.
Akitaja mashitaka mengine Kuyeko amesema, Malilo pia alimtuhumu
kuwa siku ya uchaguzi alimkuta akizungumza na msimamizi wa kituo cha Kifulu,
pia alidai uchaguzi ulikuwa na fujo.
“Hayo ni baadhi ya mashitaka ambayo alinishitaki, baada ya
mahakama kuyapitia kwa makini ilibaini kuwa ndani yake kulikuwa na uongo mwingi
pia mshitaki hakutoa ushahidi wala ufafanuzi wa kutosha kuthibitisha mashitaka
yake.
“Pia kwa hali ya kawaida mimi wa chama pinzani ni ngumu kuiba
kura kiliko yeye chama wa tawala,” amesema Kuyeko.
Hata hivyo, Kuyeko ameeleza kuridhishwa na uamuzi wa mahakama na
hivyo ametoa wito kwa mahakama zingine kutenda haki bila upendeleo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni