WIZARA YA AFYA YAJA NA MPANGO HUU,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya sekta ya afya unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, wadau hao wa Sekta ya afya wanajadiliana mambo mbalimbali na baada ya kumalizika kwa mkutano huo kutakuwa na kusaini makubaliano yaliyofikiwa kwa utekelezaji katika sekta ya afya hapa nchini , Katika picha kulia ni Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE
Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania akizungumza katika mkutano huo Kushoto ni Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
Dk.Ulisubisya Mpoki Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akichangia hoja katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Dk. Deo Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI akizungumza katika mkutano huo ambao umekutanisha wadau wa afya na kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya afya.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………………………………
NA KAROLI VINSENT
SERIKALI imesema
inatarajia kuanza kutekeleza mpango
wa mkakati wa n ne wa sekta ya Afya wa mwaka 2015 hadi 2020 utakaogharimu Sh Trion 21.
Mpango huo utajikita katika kuboresha kiwango cha ubora wa huduma katika
ngazi zote za afya ya msingi kwa
kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa
na kitita bora cha Afya na Ustawi wa Jamii.
Akizungumza leo jijini
Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa 16 wa mwaka wa mapitio ya
Sekta ya Afya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu alisema mpango huo umeainisha nikakati mitano yenye lengo la kufikisha huduma bora muhimu za afya na ustawi wa jamii katika ngazi za
kaya zote nchini.
Ametaja mikakati hiyo kuwa nii kuboresha uwiano wa
upatikanaji wa huduma bora za Afya na Ustawi
wa Jamii kwa kuondoa tofauti zilizopo za kijografia,Kiuchumi na
makundi maalum hususan Wazee,watoto
wajawazito na walemavu.
Pia kuboresha
kiwango cha ubora wa huduma
katika ngazi zote za afya ya msingi kwa
kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na
kitita bora cha afya na ustawi wa jamii.
Aidha amesema mipango
mingine ni pamoja na kuboresha ushirikishwaji wa jamii katika kupanga na
kusimamia huduma za afya katika jamii, uwekezaji katika mikakati na njia za
kisasa na ubunifu na kutambua ushiriki wa jamii na sekta nyingine katika afya.
“Tumeamua kuungana na
wadau wenzetu wa afya katika uzinduzi wa mpango mkakati utakaotusaidia kama
taifa kuiboresha na kutatua changamoto mbalimbali za afya, lakini pia
kujadiliana ni vipaumbele gani vitiliwe mkazo katika kutekeleza agenda ya
huduma za afya” amesema.
Amevitaja vipaumbele
ambavyo vimepitishwa kufanyiwa kazi ni pamoja na Kinga na Afya ya jamii,
Uwiano, Ugharamiaji wa huduma za afya, Utawala na Uongozi, Rasilimali watu
katika sekta ya afya, Dawa na Vifaa tiba, Ufuatiliaji tathimini na usimamizi wa
takwimu sambamba na utoaji wa huduma.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jaffo, alisema kuwa ikiwa ni jukumu
lao la kuhakikisha wanatekeleza sera ya
afya kwa kila mwananchi hivyo wamejipanga kujenga vituo kila kata na zahanati
kwa kila kijiji.
“Tunaona baada ya
kuanzisha mfumo wa ukusanyaji wa pesa kwa njia ya kielektroniki tumefanikiwa
kukusanya fedha nyingi katika nhospitali ya Tumbi ambayo ilikuwa ikikusanya
takriban laki mbili hadi nne,lakini tunaona hadi sasa wamefanikiwa
wanakusanya milioni tatu hadi nne kwa
siku” Alisema Jaffo.
MWISHO
Hakuna maoni
Chapisha Maoni