MAJANGILI WAISHTUA SERIKALI YA MAGUFULI,WAZIRI MAGHEMBE AUNDA KIKOSI KAZI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita baada ya Jeshi la polisi Mkoani
Simiyu kuwakamata watu 9 pamoja na mtu aliyetungua ndege (Helikopta)
iliyokuwa na ikifanya doria na kupelekea kufa kwa rubani wake
Rodger Gower (37) ,
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne
Maghembe ameibuka na kutangaza oparesheni kabambe ya kupambana na Majangili wa wanyama nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam,Waziri Maghembe huku akiambatana kwenye mkutano huo na Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini,IGP Ernest Mangu ambapo amesema kwa sasa serikali imesikitika na tukio
hilo la kinyama lilofanywa na watu anaowaita ni majangili huku akipanga kuunda
kikosi cha kazi cha kupambana na watu hao.
Amesema Kikosi hicho kitakuwa na jukumu la kupambana
na Majangili ambao wamekuwa wakiua wanyama pamoja na watu ambao wamekuwa
wakiteketeza misuti.
Ametaja Kikosi hicho kitaundwa
kwa kushirikisha Taasisi zote za Wizara (Idara ya Wanyamapori, Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Aidha,Amesema Kikosi hicho kitafanya kazi kwa karibu na Vyombo vya Ulinzi
na Usalama, Sheria, Mamlaka ya Bandari, Viwanja vya Ndege, Mamlaka ya Mapato
Tanzania, Taasisi za Uhifadhi za ndani na nje ya Nchi na wadau wengine wa
Uhifadhi;
Waziri
Maghembe amesema lengo la kikosi hicho ni kuhakikisha wanapambana na watu
wanaohusika na ujangili huku akiwataka majangili kuachana na kazi hizo kwa
madai kuwa serikali imepania kuhakikisha wanapambana na majangili hao.
Kwa Upande wa IGP Mangu amesema kwa sasa Jeshi lake
limepanga kupambana na majangili kwa
kuzipitia upya vibali vya silaha zinatumika kwa uwindaji.
“Jeshi laPolisi tumejua kuwa hawa waliopewa vibali vya silaha
kwa uwindaji ndio hawa wanatumia silaha
hizo kufanya mambo ya Ujangili,nakuhakikishieni tutazipitia silaha zote huku
zengine tukizifutia kibali chao ili kupambana na watu wanaohusika na vitendo
vya ujangili.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni