DC MAKONDA AZIDI WAMBWA MSALABANI,NI KWENYE KESI YA MBUNGE KUBENEA,SHAHIDI WAKE AJIKANYAGA,SOMA HAPO KUJUA
Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers Ltd na pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani |
DENIS Mujumba,
Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ambaye pia alikuwa Mkuu wa Upelelezi
Wilaya ya Kinondoni amefura baada ya kuulizwa maswali wakati akitoa ushahidi
wake kwenye kesi ya jinai inayomuhusu Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali
Halisi Publishers Ltd na pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo. Anaandika Faki Sosi.
Mujumba (39) amefikwa na masaibu hayo baada ya
kubanwa kwa maswali na wakili wa Kubenea, Peter Kibatala wakati akitoa utetezi
wake huku Thomas Simba ambaye ni hakimu wa kesi hiyo kwenye Mahakama ya Mkazi
Kisutu kuingilia kati na kumtaka “acha kupaniki.”
Kesi hiyo ambayo Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndio
mlalamikaji, ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya viongozi hao
wawili kugombana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar
es Salaam tarehe 14 Desemba mwaka jana.
Wakili Kibatala alimuuliza Mujumba kuwa, yeye alikutana na
baadhi askari polisi kwenye eneo la tukio, je alikuwa anawafahamu na kwamba
walikuwa chini ya nani? Mujumba alijibu kuwa aliwakuta askari hao na kuongeza
kwamba, hakufahamu askari hao na kwamba hakujua walikuwa chini ya nani.
Kibatala: Wewe ndio mwenye wajibu wa kuchunguza kesi hiyo, kwani
wewe ndio Mkuu wa Mkuu wa Idara hiyo? na kwamba siku hiyo kulikuwepo waandishi
wa habari je, ulipata ushahidi wa picha za video na sauti kutoka kwa waandshi
wa habari?
Mujumba: Ni kweli kulikuwepo na waandishi na kwamba
niliwasiliana na waandishi hao ili wanipe ushahidi wa picha, sauti au video.
Waandishi walinijibu kuwa hawana ushahidi huo.
Kibatala: je ulikwenda na askari wangapi?
Mujumba: nilikwenda na askari wanane au tisa.
Kibatala: wataje majina
Mujumba: Ni Sajenti Peter, PC Hamis, Joachim na Doel.
Kibatala: Shahidi hajui askari wake kwani anajua jina moja tu la
mwanzo na hajataja wote.
Maswali haya yalisababisha Mjumba kukunja sura na kutoa sauti ya
juu huku akitaka kubishana, Hakimu Simba alimwambia “acha kupaniki” na kumtaka
aache kubishana na wakili.
Hakimu Simba pia alimwambia Mujumba kwamba hana uwezo wa
kubishana na wakili huyo na kuwa, anachotakiwa ni kujieleza kwa kujiamini.
Wakili Kibatala kwa kutumia sheria Namba 155(a) aliiomba
mahakama kuonesha picha za ushahidi zilizokuwa zianonesha hali halisi ya tukio.
Wakili huyo aliinesha mahakama picha ambazo zilionesha kuwepo
kwa askari walioshika bunduki na kumzingira Kubena, kwenye picha hiyo Mujumba
hakuwemo.
Hapo awali Mujumba aliieleza mahakama kwamba yeye ndiye
aliyemsihi Kubenea aende naye kwenye Kituo cha Polisi Magomeni, hivyo Wakili
Kibatala aliongeza kuwa, kwa kutokuwepo kwenye picha ile Mujumba alitoa maelezo
ya uongo. Hakimu Mkazi hata hivyo, baada ya shahidi huyo kutoa ushahidi wake,
Hakimu Simba alihairisha kesi hiyo hadi tarehe 15 na 16 Aprili mwaka huu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni