BILIONI 12 ZA MAGUFULI ZAWAWEKA KITIMOTO MWAKYEMBE,MPANGO NA JAJI CHANDE,SOMA HAPO KUJUA
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa
kutimiza ahadi yake ya kuipatia Mahakama kiasi cha shilingi Bilioni 12.3
zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama na ujenzi wa Mahakama mpya katika
maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison
Mwakyembe na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto).
|
WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Philip Mpango,Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Jaji Mkuu, Othman Chande
wamekutana kwa ajili ya fedha ya Sh.bilioni 12.3 iliyotolewa na Rais John Pombe
Magufuli juu ya uendelezaji wa miundombinu ya mahakama nchini pamoja na
uendeshaji wa kesi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jaji Mkuu Othman Chande mbele ya mawaziri wa wawili, amesema fedha hiyon itakwenda katika maeneo ya utengenezaji wa miundombinu ya mahakama ili wanannchi waweze kupata haki katika vyombo vya sheria.
Jaji Mkuu, Chande amesema kuwa michoro ipo tayari kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo na wilaya ambazo hazina pamoja na mikoa ambayo hazina mahakama kuu.
Amesema adhima ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanapata haki pale wanapotaka katika vyombo vya sheria isiwe kikwazo cha kukosekana kwa mahakama katika eneo husika.
Nae Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kuwa hundi iliyotolewa jana tayari fedha hiyo imeingizwa katika akaunti ya mahakama ziweze kuanza kazi yake iliyokusudiwa.
Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwan fedha hiyo itasukuma ujenzi wa miundombinu ya mahakama ili wananchi waweze kupata haki.
Amesema hatua za ujenzi wa Mahakama ya Wahujumu Uchumi na Wala Rushwa nao uko katika hatua nzuri lakini kwa fedha hiyo ni kwa ajili uboreshaji wa miundombinu ya mahakama.

Hakuna maoni
Chapisha Maoni