IDADI YA VIFO VYA MASHABIKI WA ARSENO NA MAN U YAONGEZEKA,SOMA HAPO KUJUA
IDADI ya watu waliofariki kufuatia shambulio la
al-Shabab katika mgahawa mmoja ambapo watu walikuwa wakitazama mechi ya Arsenal
na Manchester United mjini Baidoa, Ethiopia imefika 30.
Shirika la Utangazaji la
Uingereza (BBC) limeripoti kwamba, watu 50 wanauguza majeraha hospitalini.
Mji
wa Baidoa, ambao ndio Makao Makuu ya Jimbo la Kusini Magharibi, ulikuwa chini
ya al-Shabab kabla ya kukombolewa na majeshi ya Ethiopia wakishirikiana na
wanajeshi wa Somalia mwaka 2012.
Rais
wa jimbo hilo, Shariff Hassan ameshutumu shambulio hilo na kuwahimiza wakazi
kusaidia na maofisa wa usalama.
Gari
lililotegwa mabomu lilitumiwa kulipua mgahawa wa Somali Youth League uliojaa
watu waliokuwa wakitazama mechi hiyo ya Ligi ya Premia nchini Uingereza jana
jioni. Baadaye, washambuliaji waliingia ndani.
Kwenye
shambulio la pili, mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua akiwa barabara,
eneo lenye watu wengi.
Shambulio
hilo lilitekelezwa viongozi wa mataifa yanayochangia majeshi kwenye Kikosi cha
Umoja wa Afrika nchini Somalia (Amisom) wakimaliza mkutano wao nchini Djibouti.
Viongozi
hao walikubalia kwamba, ipo haja ya kutathmini upya mkakati wa sasa wa
kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabab.
Katika
siku za karibuni, kundi hilo limezidisha mashambulio, sana likilenga kambi za
jeshi na maeneo ya umma.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni