BALOZI OMBENE SEFUE MATATANI,AANZA KUICHAFUA IKULU YA MAGUFULI,SASA ATAJWA KUWA NI JIPU KUBWA,SOMA HAPO KUJUA
KATIBU mkuu kiongozi Balozi Ombene Sefue ameanza
kuichafua Ikulu ya Rais John Magufuli baada ya kuitumia Ikulu hiyo vibaya,(Mtandao huu umedokezwa),Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo,
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya serikali
zinasema Balozi Sefue ametumia nafasi yake nyeti alikuwa nayo kumteua
mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) ,Laurean
Bwanakunu huku akiwa hana sifa ya utaalamu wa masuala ya Afya,
Uchunguzi uliofanywa na timu ya Fullhabari.blogs
umebaini mkurugenzi huyo hajasomea masuala ya afya ambayo ilitakiwa awe nayo,ambapo imebainika ana shahada ya kwanza ya
Sayansi ya Jamii (Socialogy) ,huku kwa sasa akisomea shahada ya pili katika
masuala ya sheria katika chuo cha Tumaini tawi la Dar es Salaam,.
Historia yake elimu inatia shaka kuhusika kuongoza
sehemu hiyo nyeti inakwenda kinyume na tangazo la nafasi hiyo lilotangazwa
kwenye Gazeti la Dailynews la Novemba
18,2013 lilokuwa linamtaka mwombaji awe na ufahamu wa madawa na uzoefu wa kufanya
kazi katika tasniahiyo kwa takribani kwa muda usiopungua miaka 10, jambo ambalo
mkurugenzi huyo hana sifa hizo,
Kwa mujibu chanzo chetu cha kuaminika kutoka wizara
ya Afya zinasema tangu mkurugenzi huyo
ateuliwa katika nafasi hiyo ameshindwa
kupeleka ripoti ya kitabibu wizarani kutokana na suala la elimu yake,
“Yaani ninachokwambia Rais Magufuli anaishi na Jipu
Ikulu kabisa na jipu lenyewe ni huyu Balozi Sefue yaani amelitia aibu
Taifa,huyu mkurugenzi hana kabisa elimu ya musala ya afya tena hajui hata kazi
ya dawa ndogo aina ya Metakelfini,leo
hii ndio mkururenzi wa MSD hii ni aibu kabisa”Amesema mtoa taarifa wetu aliyoko
MSD
Kuja kwa taarifa hizo kuna ikiwa ni wiki moja kupita
baada ya waziri mkuu Kassim Majaliwa kutembelea Bohari ya Kuhifadhi Vifaa vya
dawa iliyoko Mabibo Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri mkuu alienda kopekea
msaada wa vifaa uliotolewa na umoja wa
vinywaji baridi,
Inaelezwa kuwa wakati Waziri mkuu alipokuwa anakagua
vifaa hivyo mkurugenzi huyo alikuwa mbali huku akimwachia jukumu na kumtamburisha waziri mkuu vifaa hivyyo Katibu Mkuu wizara ya Afya kutokana na kutofahamu vifaa hivyo vya
kitaalamu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni