Zinazobamba

HALI YA MAUZO KATIKA SOKO LA HISA HII HAPA,SOMA HAPO KUJUA



 


 Meneja Masoko wa DSE Patrick Mususa wakati wa mkutano na waandishi wa Habari akielezea hali ya mauzo katika soko la hisa

Mauzo katika soko la Hisa DSE katika wiki hii 

Idadi ya mauzo imepanda zaidi ya mara 2 hadi Bilioni 6.3 kutoka Bilioni 2.5 wiki iliyopita.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imeongezeka zaidi ya mara 7 hadi milioni 6.6 kutoka laki 9.

Kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     CRDB kwa asilimia 93.85%
2.     SWISSPORT kwa asilimia 2.85%
3.    TBL kwa asilimia 2.38%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umebaki kwenye kiwango kile kile cha trilioni 21 wiki hadi wiki.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha trilioni 9 wiki hadi wiki.

Mabadiliko ya bei za hisa
Kampuni tatu zimeongoza katika ongezeko la bei ya Hisa zikiwa ni:
1.       KA kwa ongezeko la bei la asilimia 11.11%
2.       ACACIA kwa ongezeko la bei la asimilia 7.18%
3.       SWISSPORT kwa ongezeko la bei la asilimia 1.47%
Viashiria (Indeces)
·      Kiashiria cha sekta ya viwanda kimeshuka kwa pointi 16.75  kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta ya TCCL (10.43%), na TPCC (0.67%)
·      Kiashiria cha sekta ya huduma za kibenki na za kifedha kimeshuka kwa pointi 41.07 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta ya NMB bank kwa asilimia 4.29%.
·      Kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara kimepanda kwa pointi 41.85 kikiwa kimechangiwa na ongezeko la bei ya hisa za SWISSPORT kwa asilimia 1.47% .


Kuorodheshwa kwa bondi (hati fungani) za Exim bank
Wiki hii Hati Fungani za Exim bank, au Exim Bond, ziliorodheshwa kwenye soko la hati fungani DSE kwenye siku ya Ijumaa tarehe 26 Februari, 2016. Bondi hizi ziko sasa mnadani kwa wawekezaji ambao watapenda kuziuza hati fungani zao na kwa wawekezaji ambao wangependa kuzinunua. Bondi hizi ziliuzwa kwa Shilingi Milioni 1 kwa bondi moja ambapo kila bondi inagawa riba ya asilimia 14% kwa mwekezaji kwa kipindi cha miaka 6.

Huduma ya Kununua na Kuuza Hisa Kiganjani, *150*36#
Sasa unaweza kununua hati fungani za Exim kupitia soko la hisa kiganjani.
Kwa ajili ya kupata huduma hii, mtumiaji wa simu ya mkononi anapaswa kupiga namba *150*36# kisha kufwata maelekezo.
Huduma hii inapatikana kwa simu ya mkononi ya mtandao wowote.

Hakuna maoni