SAKATA LA MAJAMBAZI KUPORA BENKI MBAGALA,KAMANDA SIRRO ATANGAZA KIAMA,SOMA HAPO KUJUA
IKIWA ni siku moja baada ya Jeshi la Polisi kuua
majambazi watatu jijini Dar es Salaam, jeshi hilo limepanga kuanza msako wa
majambazi kwenye misitu wanakofanyia mazoezi,anaandika Regina Mkonde.
Jeshi hilo jana katika eneo la
Mbagala Rangi Tatu liliuwa majambazi waliovamia na kufanya uporaji wa fedha
zaidi ya Sh. 20 milioni katika Benki ya ACCESS Tawi la Mbagala.
Akizungumza
wakati akitoa taarifa hiyo, Simon Sirro, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam amesema, jeshi hilo pia limekamata silaha aina ya SMG moja, mabomu ya
kutupwa kwa mkono matatu, pikipiki sita na watu wanane waliokuwa wakijifanya
polisi na kukagua mabasi na kisha kuwafanyia uporaji.
“Jeshi
la Polisi Kanda ya Dar es Salaam lilifanikiwa kuua majambazi watatu ambao
hawakufahamika majina yao, katika majibizano ya risasi na polisi baada ya
kuvamia na kufanya uporaji wa fedha katika benki ya ACCESS iliyopo Mbagala
Rangi Tatu,” amesema Sirro.
Sirro
amesema, majambazi hao walishambulia kwa risasi baadhi ya wafanyakazi waliokuwa
kwenye chumba cha kuhifadhia fedha na kuua wawili.
Waliofariki
dunia ni Baraka Fredrick (25) ambaye ni mlinzi wa kampuni binafsi ya Security
Group of Africa na Abdi Salum ambaye alikuwa muuza duka jirani na benki hiyo.
“Mnamo
saa nane na nusu mchana, majambazi hao waliokuwa zaidi ya 10 wakiwa na silaha
ya SMG na mabomu ya kutupa kwa mkono, walishambulia eneo hilo kisha kukimbia,”
amesema Sirro.
Akiwa
kwenye mkutano huo Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani amesema jeshi hilo
linajipanga kufanya operesheni kwenye misitu yote ambayo majambazi hao
hujifucha na kufanya mazoezi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni