ZITTO KABWE AANZA KUICHOKA SERIKALI YA MAGUFULI,AITOLEA MANENO MAKALI,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na
kuonesha masikitiko yake kwa kitendo cha serikali kushindwa kuleta Bungeni
mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano.
Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameweka wazi jambo ambalo serikali inapaswa kufanya baada ya uchaguzi na kusema ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
"Shughuli ya kwanza ya serikali
baada ya uchaguzi ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano (
kutafsiri ilani yake kwenda kwenye mpango wa utekelezaji) . Bunge linapaswa
kujadili na kuidhinisha Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 na kisha Mpango wa mwaka
mmoja kuanza kutekeleza Mpango huo wa miaka 5. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT
Ibara ya 63(3)(c), Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 hutungiwa sheria kwa ajili ya
utekelezaji." Alisema Zitto Kabwe
"Leo Serikali ya Rais John Magufuli
ilipangiwa kuwasilisha Mpango huo wa Maendeleo wa miaka 5. Imeshindwa. Imeleta
mwelekeo wa Mpango. Haikuleta sheria na Kamati ya Bajeti Imeleta maelezo yake
kuhusu Mpango wa Maendeleo wa mwaka mmoja ilhali hakuna Mpango wa Miaka
5.
"Mwenyekiti Chenge alitaka wabunge
wajadili kwa mujibu wa kanuni ya 94 ambayo kimsingi ni Kanuni inayohusu Mpango
wa mwaka mmoja. Serikali imejichanganya. Uongozi wa Bunge
umechanganyikiwa."Aliongeza Zitto Kabwe
Zitto Kabwe alimaliza kwa kusema kuwa ni aibu kubwa
kwa serikali inayojinasibu kwa kauli ya "Hapa kazi tu"
"Bunge linapaswa kuagiza Serikali
ikalete Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 ili uidhinishwe na utungiwe Sheria kabla
ya kuanza kujadili mipango ya mwaka mmoja mmoja.
"Ni aibu kubwa kwa Serikali ya
#HapaKaziTu kushindwa kuleta Bungeni Mpango wake wa Maendeleo wa miaka 5 na
hata ule wa mwaka wake wa kwanza. Itapangaje bajeti zake? Itatekeleza vipi
ilani yake?Kuongoza nchi sio kutumbua majipu tu, ni
kuendesha nchi."Alimaliza Zitto
Kabwe
Hakuna maoni
Chapisha Maoni