WANAHARAKATI WA LHRC WACHARUKA SASA,NI KUHUSU SAKATA LA TBC LIVE BUNGE WAIBUKA NA KUIVAA SERIKALI,SOMA HAPO
Kaimu mkurugenzi wa kituo cha
sheria na haki zaBinadamu LHRC IMELDA LULU URIO akizngumza na wanahabari mapema
leo Jijini Dar es salaam kuhusu sakata lililoibuka bungeni la TBC
kusitisha matangazo ya bunge kwa sababu ya Gharama
|
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu,(LHRC)kimeingilia
kati mzozo unaendelea bungeni hivi sasa juu ya kuzuiliwa juu ya kurushwa moja kwa moja matangazo ya bunge kwenye kituo
cha TBC, ambapo wameibuka kwa kusema
Serikali imevunja katiba ya nchi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hata hivyo,LHRC pia wamelaani vikali kitendo cha
Waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo,Nape Nnauye kwa hatua ya kulifungia
Gazeti la Mawio wakidai ni muendelezo wa kuminya uhuru wa habari nchini ,
Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema jijini
Dar es Salaam, kaimu mkurugenzi wa kituo hicho IMELDA LULU URIO amesema kuwa
kusitishwa kwa matangazo ya bunge na chombo ambacho ni cha umma ni kuonyesha
dhahiri kuwa serikali haina nia ya dhati ya kuheshimu yaki ya kupata habari ya
kikatiba.
Amesema kuwa sababu zilizotolewa na waziri mwenye
dhamana ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh NAPE NAUYE kuwa kusitishwa kwa
matangazo hayo kunalenga kupunguza gharama za uendeshaji ni sababu ambazo
zinaleta maswali kuwa gharama hizi ni za nini?,na kwa ajili ya nini?na
zikitumika ni kwa manufaa ya nani?,na mchangiaji wa gharama hizi ni nani?huku
akisema kuwa TBC ni chombo cha Umma hivyo kunawajibika kwa wananchi wote bila
kujali gharama.
kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi
ambazo zimesaini makubaliano mbalimbali ya kimataifa inayohakikisha upatikanaji
wa taarifa ikiwa ni pamoja na ule wa OPG –Open government partnership
ambao ni jukwaa la serikali zenye uwazi mkataba ambao una misingi ya uwepo wa
uwazi,ushiriki,wa wananchi,uwajibikajina uweledi na ubunifu wa kutumia Tehama.
Urio amesema kitendo cha waziri Nape kulifungia
Gazeti la Mawio kunazidi kuiweka serikali ya magufuli kati mfumo wa kidikteta
ambao unaonyima uhuru wa kutoa maoni
ambao katiba ya nchi imetoa.
Amesema kuwa LHRC inaitaka serikali kutekeleza kwa vitendo
maazimio ya makubaliano ya kimataifa na kikanda katika kulinda haki ya kupata
habari na kufuta sheria kandamizi zenye kuminya uhuru huu kwa mfano sheria ya
magazeti na sheria ya makosa ya mitandao na kutunga sheria wezeshi.
Pia LHRC wameitaka serikali kuacha kuminya haki za watanzania ya
kupata habari za bunge kwa kisingizio cha gharama,na kutenga rasilimalin nyingi
kuwezesha shirika hilo waweze kuonyesha moja kwa moja matangazo ya bunge.
Tangazo la kutokuonyeshwa kwa bunge kupitia TBC lilitolewa
bungeni na waziri wa Habari NAPE NAUYE na baadae jana waziri mkuu Mh KHASIM
MAJALIWA alitoa msisitizo kuwa wameamua kusitisha matan
Hakuna maoni
Chapisha Maoni