YAMETIMA SASA,MGODI WA BUZWAGI KUFUNGWA RASMI,YALIOSEMWA NA WABUNGE WA UPINZANI YATIMIA,SOMA HAPO KUJUA
MGODI wa Dhahabu
wa Buzwagi uliopo Wilaya ya Kahama, Shinyanga unatarajiwa kusitisha shughuli za
uchimbaji (Mining) na kuendelea na uzalishaji wa maeneo ya akiba yaliyoachwa
awali kutokana na mmiliki wake kuishiwa. Anaandika Moses Mseti, Kahama … (endelea).
Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji
wa madini nchini ya Acacia, unatarajiwa kusitisha shughuli za uchimbaji
(mining) ifikapo Juni mwaka huu kutokana na mmiliki wa mgodi huo kuishiwa fedha
za kuendesha shughuli za uchimbaji.
Akizungumza jana katika ziara ya kushtukiza iliyofanywa mgodini
hapo na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano na Mazingira),
Luhaga Mpina, Meneja wa Mgodi huo, Asa Mwaipopo, amesema gharama za
kuendesha mgodi hazipo hivyo wanatarajia kutafuta mwekezaji mwingine
atakaendelea na shughuli ya uchimbaji.
Amesema kuwa ifikapo Juni mwaka huu shughuli za kuendelea na
uchimbaji (Mining) katika mgodi huo wa Buzwagi zitasimama na badala yake
wataendela na uzalishaji wa maeneo ya akiba hadi mwaka 2019 watakapofunga rasmi
shughuli za uzalishaji.
“Hatutafunga kabisa mgodi huu ambacho tutafanya ni kusitisha
shughuli za uchimbaji (mining) kuanzia Juni, lakini ile akiba ambayo tulikuwa
hatujaigusa tutaendelea nayo mpaka 2019 na kuufunga moja kwa moja na kama kuna
mwekezaji mwingine atauziwa aendelee na uzalishaji,” amesema Mwaipopo.
Hata hivyo amesema sababu zilizopelekea mmiliki wa mgodi huo
kuacha kuendelea na uchimbaji ni kutokana na kiasi cha fedha kilichotumika
katika uwekezaji kuwa kikubwa ikilinganishwa na kibachozalishwa pamoja na
gharama za kuendesha mgodi kupanda.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano na
Mazingira), Luhaga Mpina, amesema kuwa mwekezaji huyo amekomba dhahabu yote
katika eneo hilo na kuondoka nayo, hivyo hasara haitakuwa kwa mwekezaji huyo
bali itakuwa ni Taifa la Tanzania.
“Mmeondoa dhahabu yote alafu mnasema mnafunga mgodi hii ni
hasara kwa Taifa na sio kwenu, mimi nafahamu kabla ya kuwekeza lazima utafiti
wa wataalamu wenu ufanyike, hapa hakuna kufunga mgodi wala nini,” amesema
Mpina.
Mbunge wa Kahama, Jumanne Kishimba, amesema kuwa licha ya mgodi
huo kudai kwamba unaendesha shughuli zake kwa hasara lakini tatizo kubwa ni
matumizi makubwa ya fedha kwa watumishi wa mgodi huo wanaofanya kazi Kahama na
kuishi Dar es salaam.
“Kuna wafanyakazi wamegeuka miungu mtu katika mgodi huu, mtu
anafanya kazi hapa Kahama analala Dar es Salaam, anatumia usafiri wa ndege kuja
kazini unazani kuna faida watakayoipata kweli hawa,” amesema Kishimba.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni