LOWASSA AJISUKA TENA KIMAPAMBANO 2020,SOMA HAPO KUJUA
Add caption |
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza leo
kwamba anajiandaa kugombea tena urais utakapofika uchaguzi mkuu ujao Oktoba
2020. Anaandika Jabir Idrissa …
(endelea).
Lowassa ametangaza hayo mbele
ya wafanyabiashara wa sokoni Kariakoo jijini Dar es Salaam wanaojiita Team Mabadiliko, waliokwenda kumtembelea ofisini kwake
Mikocheni, Dar es Salaam.
Lowassa
amesema bado anazo nguvu na kumwezesha kugombea nafasi hiyo ya juu kabisa
katika uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hatua
hiyo inakuja wakati Lowassa akijipatia umaarufu zaidi kama mpambanaji mahiri
kisiasa, ambaye aliingia katika kinyang’anyiro hicho kwenye uchaguzi mkuu wa
Oktoba mwaka jana, akisimamia kambi kuu ya upinzani nchini.
Alijiunga
na upinzani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini akapata
kuungwa mkono na muungano wa UKAWA ulioundwa na chama hicho pamoja na Civic
United Front (CUF), National League for Democracy (NLD) na NCCR-Mageuzi.
Ugombeaji
wake ulikuja baada uamuzi wake mgumu wa kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM)
alichoanzia siasa miaka ya 1980 hadi kufikia ngazi ya Waziri Mkuu, wadhifa
aliouteuliwa kushika Novemba 2005 hadi Februari 2008 alipojiuzulu kufuatia
shinikizo la Bunge kutokana na kashfa ya mkataba tata wa umeme wa Richmond.
Lowassa
alitoa ushindani mkali katika uchaguzi mkuu kiasi cha kuaminika kuwa alipata
kura za kutosha kutwaa urais, lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
ilimtangaza mgombea wa CCM, Dk. John Magufuli kuwa mshindi. Daktari huyo wa
kemia aliapishwa rasmi Novemba 5, mwaka jana.
Umma
ulimuunga mkono Lowassa na ushahidi ukawa mikutano yake ya kampeni kufuatiliwa
na watu wengi kila alipokwenda nchi nzima. Baadhi ya maeneo mikutano
ililazimika kuahirishwa na kuandaliwa upya kutokana na wingi wa watu kutotosha
katika viwanja vilivyoandaliwa.
Lowassa
na muungano wa UKAWA walilalamika kuwa ushindi wao mkubwa uliotokana na kuungwa
mkono na umma wa Watanzania, wakiwemo maelfu ya waliomfuata Lowassa kutoka CCM,
ulihujumiwa kwa mpango mahsusi ulioandaliwa na kutekelezwa na Idara ya Usalama
wa Taifa (TISS)
Habari hii kwahisania ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni