MASIKINI STARTV,REDIO UHURU,REDIO FREE AFRIKA,KISS FM, TCRA YAZIFUNGIA RASM VIPO PIA NA VITUO VINGINE 24 VYA REDIO NA TV,NI KILIO TU,SOMA HAPO KUJUA
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imevifungia
vituo 21 vya redio pamoja vituo sita vya Television kwa mda wa miezi mitatu
baada ya kushindwa kulipia ada ya reseni.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akithibitisha kufungiwa Vituo
hivyo vya habari leo jijini Sar es Salaam wakati alipokuwa anazungumza na fullhabari.blogs,Afisa Habari wa (TCRA) Bwana Mungi amedema kuwa
Mamlaka hiyo imefikia hatua hiyo, baada ya vituo hivyo kukiuka sheria ya Utangazaji
na Posta ya Mwaka 2014 ambayo inavitaka vituo hivyo kulipia ada ya Reseni ya
Matangazo kwa kila mwaka na ada ya
masafa.
“Kifungu cha 22 cha sheria ya EPOKA ambayo ipo sura
306 na kifungu cha 21(g) inasema kuwa kampuni inaposhindwa kulipia ada ya reseni
inapewa siku 30 ili aweze kulipa lakini hawa tumewapa taarifa lakini wamekaidi
na wengine wanadaiwa tangu mwaka jana,kwahiyo ,sheria inasema wazi na sisi
tumewapa notsi ya siku 30 na bado wakawa wanasuasua kulipa, Tumevifungia kwa
miezi mitatu”Amesema Mungi.
Mungi avitaja vituo hivyo vya Redio vilivyofungiwa ni Redio Uhuru,Redio Free Afrika,Kiss Fm,Ebon
Fm,Redio Five,Country FM,Generation Fm,Impact Fm,Kill Fm,
Vyengine ni Local Fm redio,Prive Fm,Court Fm,
Sibuka FM,Standard Fm,Ulanga FM, Kifimbo,Tull Fm,Pride Fm,Redio Uhuruma,Redio
Sengerema,
Hata
hivyo,Mungi alizitaja pia vituo vya Television sita ambavyo vimefungiwa ni
StarTv,Iringa TV,Mbeya TV,Mussa Tevesion Network,Tanga Tv,Sumbawanga Tv.
Mungi ameongeza
kuwa vituo hivyo vimetakiwa kuzima matangazo yake kwaanzia usiku wa jumapili ya
terehe 17 ya mwezi huu, na endapo kituo
chochote kikaidi basi kitachukuliwa hatua kali za sheria.
Hata
hivyo,Mungi amesema endapo kituo cha chochote kitakacholipa ndani ya miezi
mitatu kwenye kifungo hicho kitafungiliwa.
“Katika kipindi cha miezi mitatu kituo chochote kikilipa
ada ya resini ,na akatimiza matakwa yote ya kisheria na akalipa pesa zote
anazodaiwa basi sisi tutamfungulia”amesema Mungi,
Vilevile Mungi amedai kuwa endapo miezi mitatu ya
kifungo hicho ikipita na vituo hivyo vitashindwa kulipa ada ya reseni basi Mamlaka
hiyo itavinyang’anya reseni ya utangazaji na kuamuliwa kuanza upya kuomba reseni.
WADAU WA HABARI WANENA.
Wakizungumza na Fullhabari.blogs wadau mbali mbali
wa habari nchini wamesema hatua ya TCRA kuvifungia Vituo hivyo ni jambo la
hatari katika ukuwaji wa sekta ya habari.
“Hapo TCRA inabidi waangalie vizuri,maana sekta ya
habari Tanzania ni ngumu sana tofautisha na nchi ya Kenya,wenzetu wale
wanaviwanda vingi sana,viwanda vile vinapeleka bidhaa kwenye vyombo vya habari
kutangaza na redio zinapata pesa,sasa hapa nchini hakuna viwanda kwahiyo media
zinang’ang’ania matangazo tigo,voda tu,wewe unategemea nini,vitakufa vingi tu”amesema
Jackson Maliasi Msomi wa masuala ya habari kutoka chuo kikuu huria
Hakuna maoni
Chapisha Maoni