UKAWA WAIBUKA KIDEDEA UMEYA ILALA NA KINONDONI,CCM NA NA MAMLUKI WAO WAULA WA CHUYA,SOMA HAPO KUJUA
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob (katikati) akiongoza sala ya kufungua mkutano wa kwanza baada ya uchaguzi wa kumchagua Meya na Naibu Meya wa manispaa hiyo. |
HATIMAYE baada ya danadana za muda mrefu, uchaguzi
wa kuwachagua Mameya wa Manispaa za Kinondoni na Ilala, umefanyika na Umoja wa
Vyama vinavyodai Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamefanikiwa kuongoza Manispaa
hizo. Anaandika Sarafina Lidwino …
(endelea).
Chaguzi hizo zilizhairishwa
mara mbili kutokana na mvutano uliotokewa katika chaguzi za nyuma, ikiwa pamoja
na kusimamishwa kwa amri za mahakama.
Kwa
upande wa Manispaa ya Kinondoni, Diwani wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema,
Boniface Jacob amefanikiwa kuwa Meya wa manispaa hiyo baada ya kushinda kwa
kura 38 dhidi ya mpinzani wake, Benjamin Sitta wa CCM aliyepata kura 2o. Naibu
Meya ni Diwani wa Tandale kwa tiketi ya CUF, Jumanne Ameir Mbunju.
Uchaguzi
wa Manispaa ya Ilala ambao leo pia uliingia katika mgogoro kati ya
madiwani wa CCM na wale wa Ukawa, hali iliyosababisha CCM kususia uchaguzi huo
na kuwaacha Ukawa kupiga kura peke yao na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
kumtangaza mshindi kuwa Meya wa Ilala ni Charles Kuyeko (Chadema) amepata
kura 31, wakati Naibu Meya ni Omary Kumbilyamoto (CUF) amepata kura 31.
Jumla
ya madiwani waliotakiwa kupiga kura katika uchaguzi huo ni 54, hivyo madiwani
31 wa Ukawa waliobaki ndani walitimiza akidi ya uchaguzi huo kuendelea.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni