WAZIRI NAPE ATAJA SABABU YA KULIFUNGIA GAZETI LA MAWIO,WAMILIKI WAKE WAIBUKA WASEMA WATALIFUNGUA JENGINE,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI wa Habari,utamaduni,sanaa na michezo,Nape Nnauye akizngumza na wanahabari Mapema Leo Jijini Dar es salaam kuhusu kulifuta Gazeti La mawio katika Orodha ya magazeti nchini Tanzania |
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Habari,utamaduni,sanaa na michezo,Nape Nnauye
ametaja sababu ya serikali kulifuta Gazeti la Mawio kwenye orodha ya msajili wa
magazeti nchini kwa kusema wahariri wa
Gazeti hilo wa wamekuwa na kiburi kwa
serikali wanapotakiwa kujitetea kuhusu habari wanazoandika.
Akizungumza na waandishi wa habari mda huu jijini
Dar es Salaam,waziri Nnauye amesema serikali imefikia hatua ya kulifuta gazeti
hilo kwenye orodha ya msajili wa magazeti pamoja na kulizuia kutochapishwa
kwenye mitandao baada ya kutolidhishwa na mienendo yake.
“Sheria ya magazeti ya mwaka 1976 sura ya 229
kifungu cha 25 (i) kinamenipa mamlaka ya kulifungia gazeti hili,kwahiyo kwaanzia tarehe 15 January mwaka huu
tumelifuta kwenye orodha ya magazeti ya
msajili,kwahiyo tumelipiga marufuku hata kuchapisha kwenye mtandao’amesema
Waziri.
Waziri Nnauye ameyataja makosa yaliyopelekea
serikali mpaka kuchukua hatua hiyo,ni baada ya ofisi ya msajili wa magazeti kuwaandikia
barua wahariri wa gazeti hilo kwa kuwataka kusahihisha makosa yao tangu mwaka
2013 jambo analodai kuwa wahariri wake walikuwa wanaijibu majibu mabaya
serikali.
“Yaani wahariri wa hili gazeti tangu mwaka 2013
tunawaambia wabadilishe aina ya uandishi wa habari lakini wakawa wanaijibu
serikali majibu mabaya na wakawa wanaendelea kuandika habari ya uchochezi na
kuharibu amani ya nchi,”
Hata hivyo,Waziri Nnauye amevitaka vyombo vya habari
pamoja na wahariri kuzingatia sheria na kanuni za taratibu za nchi kwa kuandika
habari zenye kufuata weledi.
WAHARIRI
WA MAWIO WANATAFUTWA.
Taarifa ambazo Fullhabari.blog imezipata zinasema Jeshi la Polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam linawatafuta wahariri wa gazeti la mawio ambao ni Saimon Mkina
na Jabir Idrissa kwa kosa la kuandika habari inayodaiwa ni yenye uchochezi
kwenye gazeti hilo toleo 152 ya Alhamisi
ya tarehe 13 mwezi junuary mwaka huu yenye kichwa cha habari MACHAFUKO YAJA
ZANZIBAR.
‘Ninachokwambia tangu juzi ijumaa wamekuja polisi
wamevamia kwenye ofisi zetu mbili za magomeni na ile ya pale mwananyamala
wanakuja kuwasaka hawa wahariri wetu na wamewakosa”amesema mtoa taarifa wetu wa
Gazeti la Mawio
.
.
MMILIKI WA
MAWIO ANENA.
Akizungumza na Fullhabari.blogs kwa sharti la
kutotaja jina lake Mtandaoni mmliki mmoja wapo wa Gazeti hilo,amesema kwa sasa
wanajipanga kulifufua gazeti moja wapo ambalo litaendelea na kazi zilizokuwa
zikifanywa na gazeti lililofungiwa .
“Tumepokea kwa masikitiko makubwa kwa kufungiwa
gazeti letu,ila tupo mbioni kufufua gazeti moja wapo lilokufa,na kuhakikishia
alhamisi tunaendelea tena utashangaa ndugu”
Aidha akijibu kuhusu swali la mwandishi wa habarti
alilotaka kujua kama wanaruhusiwa kufungua gazeti lingine au kulifufu gazeti moja wapo lilokufa na kuendelea na kazi
waziri NAPE amesema kuwa sheria inaruhusu mtu kufungua gazeti na hawana
kipingamizi japo hakuweka wazi hatua ambazo watachukua kama wakifungua na
kuendelea kufanya hivyo.
“Tunajua wanaweza kufanya hivyo,kwani hata Gazeti la
Mwanahalisi lilipofungua siwakaja kwa mlango wa Mawio,na sisi tunawaambia
wafanye hivyo kama wanataka sisi hatuna pinga mizi kwakuwa sheria si inaruhusu
wafanye tu”amesema Waziri Nape
Hakuna maoni
Chapisha Maoni