WAZIRI WA MAGUFULI ATUMBUA MAJIPU BANDARINI,AWAONDOA VIGOGO,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano,Profesa
Makame Mbarawa amewahamisha kazi watendaji wa juu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA)
baada kuisababishia serikali hasara kwenye upotevu wa makontena katika bandari
hiyo.
Watendaji
hao waliohamishwa kazi ni, Piter gawilo
ambaye alikuwa mkurugenzi wa Rasilimali
watu ndani ya Mamlaka hiyo,ambaye
ameondolewa kwenye nafasi hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Antony Mbilinyi
ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa Rasilimali watu ndani ya Mamlaka ya
Mawasiliano nchini (TCRA).
Wengine ni
waliomishwa Kazi ni Kaimu mkurugenzi wa manunuzi wa TPA, Mashaka Kishanda ambaye
nafasi yake nafasi yake imechukuliwa Benito Kalinga ambaye awali alikuwa mtumishi wizarani hapo,
Sanjari
hao, mwengine aliohamishwa ni Kaimu mkurugenzi wa TEHEMA wa TPA,Kalian Charles
naye nafasi yake imechuliwa Abdullhaman
Bamba ambaye awali naye pia walikuwa wizarani ya ujenzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri Mbarawa amesema nia ya
serikali ya kuwaondoa watendaji hao ni kukata kuongoza kasi ya ukusanyaji mapato
ndani ya TPA.
“Serikali
imefuikia uaamuzi huu,kwa lengo la kuongeza kasi ya ukusanyaji kodi kwenye
Mamlaka ya Bandari ndio maana tumewaondoa watendaji hawa tumewaweka watu ambao
watazidisha kasi ya ukusanyaji mapato “amesema Waziri Mbarawa.
Hata hivyo,Waziri Mbarawa amesema watendaji hao
waliondolewa kwenye nafasi hizo,wamerejeshwa wizarani na kusubuli kupangiwa
kazi nyengine.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni