MAGUFULI ACHARUKA AIFUNGIA KAMPUNI YA SIMU,PIA AZIFUNGIA REDIO 28 NCHINI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani wa kati kati ni Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Masiliona,Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaa |
NA KAROLI VINSENT
SERIKALI nchini imetangaza kuifungia kampuni ya simu
ya six Telecom pamoja na kuifungulia jarada la kiuchunguzi polisi, baada kubainika
kuwa ilikosesha serikali mapato yaliyotokana na kodi yanayofikia bilioni 8.5
pamoja na kutoza gharama ya simu kwa
wateja kwa kiwango cha chini
tofauti na ile iliyopangwa na serikali.
Hata
hivyo,Serikali pia imetangaza kuzifungia redio 28 nchini baada ya kushindwa
kulipia ada ya reseni.
Akitangaza
uaamuzi huo,leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi,Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa amesema serikali imefikia uamuzi wa
kuifungia Kampuni hiyo ya simu baada ya
kufanya makosa mbali mbali,
Waziri Mbarawa
ameyataja makosa hayo kuwa ni kuikosesha
mapato serikali yaliofikia billion 7.2 na kukataa kulipa ada ya reseni ambayo ni bilioni
1,pamoja na kugoma kulipa toza ya faini ya milioni 361.25
“Kwaanzia
sasa tumeifungia kampuni hii ya Six Telecom baada ya kukiuka sheria mbalimbali
ambapo Kampuni hii ya simu ilisajiliwa kutoa huduma mwaka 2013,lakini ikaanza kukiuka kanuni za Mamlaka ya mawasilioni nchini (TCRA) ambayo
iliweka kiwango cha chini cha gharama
kwa kupiga simu nje ya nchi wakati ilitakiwa kutoza gharama kubwa,”
“Licha kutoza
kiwango hiki cha chini ya kiwango pia imeshindwa kulipa kodi ya Bilioni 7.2 pamoja na kukataa kulipa gharama za reseni inayofikia bilioni 1 na
kushindwa kulipa faini ya milioni 361.25
iliyotokana kukiuka kanuni za huduma
hiyo”amesema Mbarawa.
Vilevile,Waziri
Mbarawa ametangaza kuzifungia rasmi redio 28 nchini baada ya kushindwa
kulipa ada ya reseni kwenye Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA
jambo analodai kuwa ni kosa.
“Tumezifungia redio 28 ambazo Kesho (TCRA)
watazitaja kwa majina,kwani redio hizi zimeshindwa kulipa ada ya reseni ambapo kisheria
wanatakiwa kulipa,lakini redio hizi zilishindwa kulipa ”amesema Waziri Mbarawa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni