NI MUNGU TU NDIYE ATAKAYE MUOKOA ZITTO KABWE KWENYE KUPEWA CHEO CHA PAC,SAKATA LA ESCROW KUMPONZA,SOMA HAPO KUJUA
MBUNGE wa Kigoma Mjini kupitia chama cha
ACT-Wazalendo,Zitto Kabwe,jina lake limeondolewa kwenye nafasi ya uwenyekiti wa
kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC).(Mtandao umedokezwa).Aaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kabwe ambaye alidumu kwenye nafasi ya hiyo wakati Bunge
la kumi lilopita,ambapo kwa sasa alijiapiza kurudi tena kwenye nafasi hiyo
nyeti ndani bunge ambapo inaonekana ni kama ndoto yake imeota mbawa.
Taarifa za
kuaminika kutoka ndani ya Ofisi za Bunge ambazo mtandao huu umezipata zinasema
Spika Job Ndugai ameshamaliza kupanga
safu kwenye kamati mbali mbali, kabla
haja wasilisha majina hayo,kwenye kamati itakayokutana
kesho ijumaa ya tarehe 15 kwenye kikao cha kamati itakachofanikia ofisi ndogo za
Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupitisha majina hayo ya
viongozi wa kamati mbali mbali za Bunge na wajumbe wake,
Ambapo inatakatiwa wajumbe wa kamati na wenyekiti
wake kumalizika na uteuzi wake kabla ya
kikao cha Bunge akijaanza tarahe 26 ya mwezi huu.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu huyo ameuambia mtandao
huu jina la zitto Kabwe limeenguliwa kwenye kamati ya (PAC) kwa kile
kinachoitwa ni kutokana na tuhuma mbali mbali alizotumiwa wakati akiwa
mwenyekiti wa (PAC).
“Spika Ndugai alishakamilisha safu yake siku nyingi
sana,katika safu za kamati ndani ya Bunge,kuhusu PAC jina la zitto alipo lilishaondolewa
kabisa,nakuapia kabisa ndugu huyu Ziito ategemee Mungu tu kurudi kwenye Kamati
ya PAC”Kimesema Chanzo chetu hicho.
Inadaiwa Zitto anatarajiwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati moja wapo
tofauti na PAC ambapo mtoa taarifa wetu aligoma kutaja kwa kusema ni bado mapema huku akimtaka
mwandishi wa mtandao kuwa na subira.
Sababu
inayotajwa na vyanzo mbali mbali kutoka ndani ya Bunge ni kuwa Spika Ndugai amefikia
uamuzi huo wa kumwondoa Zitto Kabwe kwenye PAC
inatokana na wabunge wenzake haswa wa Upinzani kujiandaa kumgomea zitto kurudi
nafasi hiyo baada ya kutuotuhuma mbali mbali anazotuhimiwa wakati akiwa
kiongozi wa kamati hiyo,
Tuhumu
hizo ni ile ya kuilinda serikali wakati Kamati yake ilipokuwa inachambua ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakati ilipokuwa
inachunguza sakata la uchotwaji wa mabilioni ya escrow iliyokuwa ndani
ya Benki kuu B.OT,
Ambapo Zitto Kabwe anatuhumiwa kwake kwa kushindwa
kutaja majina ya Vigogo waliopewa mgao wa fedha na anayejiita na Kuitwa mmiliki wa kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP)
bwana Seith kwenye Benki ya stanbink ambao inadaiwavigogo wakubwa wa serikali
pamoja na watendaji wa kipindi kile wa Ikulu walinufaika na mgao huo
,Huku Zitto akaishia kuwataja wahusika walipewa mgao
na mmiliki wa kampuni ya Engineering and Marketing Limited (VIP) James
Rugemalira kupitia Benki ya Mkombozi.
“Zitto huyu mwenyewe amejiaharibia wakati
akiwa mwenyekiti wa PAC alikubali kuwatoa kafara wakina Tibaijuka watu ambao
hata hawaijuia Escrow yenyewe,akawafumbia macho vigogo wa Stanbick huku ndiko
hadi watu wa ikulu walikula, ambapo kamati yake PAC ilikuwa na Nguvu ya kuitaka
TAKUKURU kuwapa majina ili wajulikane wakina nani lakini yeye hakufanya hivyo
sasa leo ndio anavuna alichopanda kabisa na Spika kaangalia huyu mtu aaminiki”
Alipotafutwa Zitto
Kabwe ili ajibu hatua hii ya Spika kuliondoa jina lake,simu yake Haikuweza kupatikana.
Akizungumzia hatua ya Spika Ndugai kuliindoa jina
lake,Mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoa chuo kikuu cha Dodoma William Alocye
amesema hatua hiyo itakuwa pigo kubwa kwa Zitto Kabwe.
“Yaani hapo naiona dalili ya zitto kabwe kupotea
umaarufu wake,maana kamati hiyo imempa umaarufu sana na pia sio hivyo tu hata
kipesa amenufaika maana hapo kuna mengi sana yamefichika ndugu huyo anakagua
mashirika ya umma unategemea nini kwa mashirika ya umma yanavyonuka ufisadi
hivyo yeye unategemea naye asinufaike”amesema Alocye.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni