WAZIRI NAPE AENDELEA KULICHAFUA BARAZA LA MAWAZIRI LA MAGUFULI,MZIMU WA GAZETI LA MAWIO WAMTAFUNA,ACHAFUA HALI YA BUNGE,SOMA HAPO KUJUA
VIONGOZI wa
Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba (Ukawa), wakiongozana na Mbunge wa Kigoma
Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), walieleza kwamba kamwe hawataacha serikali
iendelee kupoka haki ya kikatiba ya wananchi, kwa kuwazuia kutoa na kupata
habari. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Viongozi hao waliwanyooshea vidole wabunge wa
CCM kwamba ni wanafiki, kwa sababu wakati wao (wapinzani) wakijadiliana na
Kamati ya Uongozi wa Bunge, walikuwa wakipokea ‘vimemo’ wakiwaomba waendelee
kupambana kwa sababu hata wao hawapendi yanayoendelea kufanywa.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Mwenyekiti mwenza wa
Ukawa, Freeman Mbowe, amesema wanalaani udharirishwaji waliofanyiwa
wabunge wa upinzani bungeni, kwa kutumia askari wenye silaha mbalimbali
na mbwa, kwamba ni ukiukwaji wa haki za bunge.
Amesema sababu zilizotolewa na serikali kuzuia Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), kurusha moja kwa moja matukio ya bungeni hazina
mashiko na kwamba wamebaini mambo matano yanayoipa kiwewe mpaka kufikia hatua
hiyo.
Hata hivyo amesema hawajasusia vikao vya bunge, leo wataendelea
kushiriki shughuli za bunge kama kawaida lakini wakiendelea kudai haki za
kikanuni na kikatiba kuzingatiwa, kwa maslahi ya watanzania wote.
Ametaja mambo hayo kuwa ni mjadala kuhusu hali ya kisiasa
Zanzibar, kasoro zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu uliyomalizika Mwaka 2015,
maamuzi yanayochukuliwa na baadhi ya viongozi wa serikali ya awamu ya tano,
bila kuzingatia sheria, taratibu na kanuni mbalimbali kwa kisingizio cha
‘kutumbua majipu’.
Kiongozi mwingine wa Ukawa, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia
(NCCR-Mageuzi) amesema wabunge wengi kwa sasa wanaofanya siasa za kizazi kipya,
hawatakubali kurudishwa enzi za ‘zidumu fikra za mwenyekiti’.
“Tuko tayari kuuawa sote lakini ifahamike hilo likitokea,
wengine wataendelea kujitokeza kuendeleza madai mpaka haki itakapopatikana,”
alieleza Mbatia.
ZITTO AFUNGUKA KUHUSU NAPE
Hakuna maoni
Chapisha Maoni