WAZIRI KAILUKI AUANGUKIA MFUKO WA RAIS KUHUSU TATIZO LA AJIRA KWA WAHITIMU WA CHUO KIKUU,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI wa
nchi ofisi ya Rais ,Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala
bora,Angella Kairuki amewataka watendaji
wa mfuko wa Rais wa kujitegemea (PTF) kuangalia uwezekano wa kuwawezesha wanafunzi
wanaomaliza chuo kikuu ili waachane na fikra za kutegemea kuajiliwa badala yake
wawe na fikra za kujiajiri.Anaadika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Waziri
Kailuki amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara kwenye
ofisi za mfuko huo,ambapo amesema nia ya serikali ya kuanzisha mfuko huo ni
kuwawezesha wananchi,lakini amewataka kuacha kuwaangalia peke yao wanafunzi
wanohitimua katika vyuo vya ufundi pekee yao kama wanavyofanya sasa.
“Kwa sasa
kumekuwa na wanafunzi wengi wanaomaliza chuo kikuu wanakuwa hawana ajira huku
fikra zao zinategemea kuajiriwa cha msingi hapa ni kuacha kuwafikilia
wanaomaliza vyuo vya ufundi sahivi ni kuweka mkazo kwenye vyuo vikuu ili tuweze
kuwaokoa na dhana ya kuajiriwa”amesema Waziri Kailuki.
Waziri Kailuki amesema kwa sasa mfuko huo kasi yake
iliyotegemewa wakati inaanzishwa kwenye miaka ya 1984 kwa lengo la kuwawezesha wanatanzania
waweze kujikwamua na hali ngumu ya maisha kutokana na viongozi wa mfuko huo
kukosa utawala bora jambo aliloitaka bodi hiyo mpaka kufikia tarehe 5 ya mwezi
ujao wawe wamepelekea sera ya ufanyaji kazi,
Ambapo amedai sera hiyo ikishaaandaliwa itapelekea
kupunguza tatizo la urasimu kwa wananchi
wanapotaka huduma.
Awali akimkaribishwa Waziri, Mkuregenzi wa mfuko
huo,Haigath Kitala amesema mfuko huo umeshindwa kufikia malengo yake ya
kuwawezesha wajasiliamali kwa asilimia kubwa kutokana na kuelemewa na madeni
jambo analodai limechangia mfuko huo kuwa nyuma.
Amedai kuwa licha ya kuwa na madeni hayo,pia hata
Bajeti inayotengwa na serikali imekuwa ndogo ambayo hawezi kukidhi uendeshaji
wa mfuko huo,sanjari na kukosa watumishi wa idara mbali mbali katika mfuko huo,
Akizungumia Changomoto hizo,Waziri Kailuki
amewakikishia watendaji wa mfuko huo
kuwa atazifanyia kazi changomoto zao ili mfuko huo uondekane na tatizo hilo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni