TAARIFA MUHIMU KUHUSU UKWELI JUU YA KUONDOLEWA JENERALI MWAMUNYANGE NA RAIS MAGUFULI KWENYE NAFASI YAKE,SOMA HAPO KUJUA
RAIS John Magufuli amemwongeza mda wa mwaka
mmoja,Mkuu wa majeshi ya ulinzi
nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya
kutimiza umri kwa mujibu wa katiba na
sheria.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza na waandishi wa habari,leo mapema kwenye
Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)yaliyopo Upanga jijini Dar es
salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa
Jeshi ya ulinzi nchini pamoja na Meneja
Jenerali wawili, ambapo wote kwa pamoja kwa pamoja wamestaa ndani ya Jeshi kwa mujibu wa
sheria ya jeshi hilo.
“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 31
Januari,2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi
jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 31 januari,2016 hadi tarehe 31 Januari 2017,”amesema Jenerali Mwamunyange
Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais
Magufuli kumwongezea mda huo,imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza
nafasi hiyo aliyonayo tena.
Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli
amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo
kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi,
Sanajari
na huyo,Jeneral Mwanunyange amesema pia,Rais Magufuli , amefanya uteuzi mkubwa
ndani ya Jeshi hilo ili baada ya kuteua watu kushikanyadhifa mbali mbali ndani ya jeshi hilo,
Jenerali
Mwamunyange ametaja walioteuliwa na Rais, ni Meja Jenerali James Aliois
Mwakibolwa kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi
la nchi Kavu,ambaye amechukua nafasi ya meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu
anayestaaafu kazi leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria,ambapo Meja
Mwakibolwa alikuwa ni mkuu wa tawi la utendaji wa kivita na mafunzo makao mkuu
ya jeshi.
Jeneral Mwamunyange alimtaja pia aliyeteuliwa na
Rais,ni -Meja Jenerali-Yakub Sirakwi kuwa Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant
NDC) - kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na
Rais kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Maliasilia na utalii,Meja Jenerali Sirakwi
alikuwa mratibu msaidizi mkuu baraza la usalama wa Taifa- BUT.
Mwengine ni aliyeteliwa na Rais Magufuli ni -Brigedia
Jenerali George William Ingram, kuwa Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga, ambaye aliyechukua
nafasi ya Meja Jenerali Joseph Pwani aliyestaafu leo kisheria baada ya kufikia umri wa kustaafu,Bregedua
Jenerali Ingram alikuwa Afisa Mnadhimu katika mako makuu ya kamandi ya Jeshi la
Anga.
Pia Rais Magufuli alimteua Bregedia
Jeneralio M.W Isamuhyo kuwa Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa-,kuchukua
nafasi ya Meja Jenerali Raphael Muhuga anayestaafu kazi leo, baada ya kufikisha
umri wa kustaafu kazi kisheria,kabla ya uteuzi Bregedia Isamuhyo alikuwa
mkurugenzi makao mkuu ya jeshi.
Vilevile Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali
Jacob Kingu kuwa mkuu wa
shirika la mzinga-,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Charles Muzanila
anayestaafu leo kisheria baada ya kufikisha umrii,Brigedia Jeneral Kingu
alikuwa mkuu wa utawala na mafunzo katika makao mkuu ya jeshi la kujenga Taifa.
Hata
Hivyo,Rais Magufuli amemteua Bregedia
Jenerali Robison Mwanjela, kuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS)- kuchukua
nafasi ya Brigedia Jenerali Msangi anatestaafu leo kazi,baada ya kufikisha umri
kustaafu kisheria,Kabla ya uteuzi Brigedia Jeneral Mwanjela alikuwa mkuu wa
Tiba Hopsitali kuu ya Jeshi Lugalo.
Aidha,Rais
Magufuli amemteua Brigedia Jeneral George Msongole kuwa Kamanda
wa Brigedia ya Tembo,- kuchukua nafasi ya Brigedia Jeneral J.M Chacha ambaye
anastaafu leo baada kisheria baada ya kufikisha umri wa kustaafu,Bregedia
Jenerali Msongole kabla ya kustaafu alikuwa bAfusa Mnadhimu makao makuu wa
Jeshii.
Rais
Magufulia pia amemteua Bregedia Jenerali
Sylevesta M.Mijna kuwa mkuu wa chuo cha ukamanda kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Ezekiel
Kyunga ambaye anastaafu kzai leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu
kisheria,ambapo kabya ya uteuzi,Bregedia Jenerali Minja alikuwa mkuu wa utawala
katika chuo cha Ulinzii wa Taifa –NDC.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni