NARCO YAANZA KUWAFURUSHA WALIOVAMIA MAENEO YAO... YATOA SIKU 30 KWA WALIOVAMIA RANCHI YA RUVU KUHAMA...
Kaimu meneja mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Tifa (NARCO) Bwire Kafumu, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika eneo la Ranchi Ruvu. |
Kamati ya ulinzi na usaklama wilaya ya Bagamoyo, wakiwa katika kikao, kijiji cha Kidogozero, kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze. |
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majidi Hemed Mwanga, mwenye miwani akitafakari baada ya msafara wake kunasa kwenye tope katikati ya msitu wa Ranchi ya Ruvu |
Na Athumani Shomari- Bagamoyo.
Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imetoa siku 30 kwa watu
wote walovamia Ranchi ya Ruvu iliyopo kata ya Vigwaaza wilayani Bagamoyo
kuondoka kwa hiyari katika eneo hilo.
Tamko hilo limetolewa na kaimu meneja mkuu wa Kampuni ya
Ranchi za Taifa, Bwilre Kafumu alipokuwa akitoa taarifa ya uvamizi wa ranchi ya
Ruvu mbele ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.
Kafumu amesema Ranchi hiyo ambayo ni moja kati ya Ranchi 14 zilizopo
chini ya umiliki wa Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO imeanzishwa mwaka 1956 na Shirika la Kilimo
Tanganyika TAC na baada ya hapo mwaka 1961 ilichukuliwa na wizara ya kilimo
chini ya Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO.
Kafumu, amesema kuwa, NARCO ina mipango ya muda merfu, muda
mfupi muda wa kati, ambapo mipango ya muda wa kati ni pamoja na ujenzi wa
machinjia ya kisasa inayojengwa Ruvu ambayo inatarajiwa kuchinja Ng’ombe elfu
thelasini, 30,000 na mbuzi elfu themanini 80,000 kwa mwezi.
Ranchi ya Ruvu imekumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo
kuvamiwa na wanachi wanofanya shughuli mbalimbali ndani ya eneo hilo ikiwemo
ufugaji, kilimo na ukuataji mkaa, ambapo sasa wametakiwa mpaka kufikia tarehe
26 mwezi wa pili wawe wameondoka katika eneo hilo.
Eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 44,000 limezunguukwa na
vijiji vilivyopo kata ya Vigwaza katika Halmashauri ya Chalinze vikiwemo vijiji
vya kwa Zoka, Buyuni, Kitonga, Kidogozero na Mkenge, ambapo wananchi wa vijiji
hivyo kupitia serikali zao za vijiji wameiomba serikali kutafuta uwezekano wa
kuwaongezea eneo kutoka NARCO ili waweze kufanya shughuli za kilimo na makazi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Hemedi
Mwanga amewataka viongozi wa vitongoji na vijiji kuorodhosha majina ya wananchi
wenye mahitaji ya ardhi na kuyawasilisha kwenye mkutano wa kijiji ambao
utahudhuriwa na mkuu wa wilaya, ili kuona uwezekano wa kuomba eneo kutoka
NARCO, huku akiwaonya wenyeviti wa vijiji kuepuka udanganyifu katika zoezi
hilo.
Amesema katika zoezi hilo majina yote ya wahitaji wa aridhi
yatapitiwa mbele ya mkutano mkuu wa kijiji husika na kwamba mwenyekiti atakae
orodhesha jina ambalo sio la mkazi wa kijiji husika atachukuliwa hatua za
kisheria.
Majidi amesema wenyeviti wengi wana tabia ya kuuza maeneo ambapo
amewaonya wenyeviti wa vitongoji au vijiji wenye tabia hiyo waiyache mara moja
vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.
Aidha, mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa watu wote
wanaotaka Aridhi Bagamoyo kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kufika ofisi za
aridhi ili kupewa maelekezo ya eneo gani limetengwa kwa kazi gani badala ya
kuuziwa na watu ambao hawajui aridhi husika imetengwa kwa kazi gani.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo amefanya ziara ya kutembelea
vijiji vinavyopakana na Ranchi ya Ruvu ili kupokea mahitaji ya aridhi kutoka
kwa wananchi wa vijiji hivyo na kuyawasilisha kwa kampuni ya ya ranchi za taifa
ili kuona kama kuna uwezekano wa kuwaongezea wananchi eneo kwaajili ya shughuli
za kilimo na mifugo, na makazi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni