SAKATA LA KUFUNGIWA GAZETI LA MAWIO LAZIDI CHUKUA SURA MPYA TENA,JUKWAA LA WAHARIRI NA MBUNGE KUBENEA WAMTANGAZIA KIAMA WAZIRI NAPE,SOMA HAPO KUJUA
HATIMAYE Wahariri wa Gazeti la Mawio ambao walikuwa
wanatufutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Ya Dar es Salaam wamejisalimishwa kwenye Makao mkuu ya Kanda hiyo.Aaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo
Wahariri hao ni Jabir Idrisa,Saimon Mkina wamejisalimisha
mda wa saa 8.56 mchana jijini hapa,huku wakiongozana na Mwanasheria wa Gazeti
hilo Frederick Kihwelo na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri nchini (TEF),Absalom
Kibanda,Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea,Aliyekuwa mhariri mtendaji wa Gazeti la
Tanzania Daima,Ansbert Ngurumo.
Gazeti la Mawio
ambalo lilifungiwa mwishoni mwa wiki
iliyopita na Waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo ,Nape Nnauye kwa
kutumia sheria kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976 kwa kusema kuwa Gazeti hilo
lilikuwa linaandika habari za uchochezi.
Akizungumza nje ya Polisi hapo mara baada ya wahariri hao
kujisalimisha,Mwenyekiti wa TEF,Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa
magazeti ya Mtanzania,Dimba,Rai nguvu ya hoja,The African,Bingwa,amewambia
waandishi wa habari, kuwa wao kama (TEF) wamekuja kumsindikiza mhariri
mwenzao polisi hapo kwa madai kuwa ni miongoni mwa wajumbe kwenye jukwaa hilo.
“Tumekuja kuwasindikiza wenzetu hawa kwakuwa ni wajumbe wa
TEF,tumekuja pia kujua sababu gani ya
polisi kuwaita wahariri hawa”amesema Kibanda.
Hata hivyo
Kibanda alitumia nafasi hiyo kutoa masikitiko yake kwa hatua iliyochukuliwa na
serikali kwa kulifungia Gazeti la Mawio kwa kusema serikali inanyima uhuru wa
habari kwani wao kama TEF hawaoni kosa walilofanya Gazeti hilo mpaka kupewa
adhabu hiyo kubwa.
“Tumesikitika
sana na hatua hii ya kikandamizaji ya kulifungia Gazeti la Mawio na huu ni
mwendelezo wa serikali kunyima uhuru wa habari nchini,na sisi jukwaa la
wahariri hatutakubali kufanya kazi na waziri wa aina hii na tutatoa tamko
ngojeeni”amesema kibanda.
Kwa upande wake Mbunge wa Ubungo wa Saed Kubenea,ambaye pia
ni mkurugenzi wa Kampuni ya Hali halisi limited ambayo inamiliki Gazeti la
Mwanahalisi,Mtandao wa Mwanahalisi oline,Gazeti la Mseto,amesema amekuja Polisi
hapo ili kwasababu miongoni mwa wahariri alishikiliwa na polisi ni mfanyakazi
wake.
“Huyu Jabir ambaye amejisalimisha leo ni mfanyakazi wangu
kwenye Gazeti la Mwanahalisi na nimeshangaa kwanini leo polisi naye wamemkatamata hili ni jambo la ajabu sana na huu ni uonevu unaofanywa na serikali ili kutaka
kuwaziba wanahabari mdomo wasisema mamba mabaya kwa serikali”amesema Kubenea.
Kubenea pia alikusita hatua kuzungumzia hatua ya serikali
kulifungia gazeti la Mawio kwa kusema Waziri Nape amekurupuka na anafanya kazi
ya katibu uenezi wa chama cha Mapinduzi CCM kwenye nafasi ya uwaziri.
“Huyu Waziri amekurupuka tu hakuna kosa lolote Gazeti
lilofanya,anasema Gazeti limeandika uchochezi, hivi wanahabari mtu wakusema
habari hii ni ya uchochezi ni Mahakama na sio waziri wa habari,nashangaa yeye
anasema tumeandika uchochezi wakati sio mahakama”amesema Kubenea.
Kubenea ameongeza kuwa Waziri Nape anapodai Gazeti la Mawio
linaandika Uchochezi amedai kuwa ni
uongo wa mchana kwani kama lingekuwa linaandika uchochezi mbona waziri huyo
alikuwa anaandika habari kwenye gazeti hilo.
“Huyu Nape leo anafanya kugeuka mbona alikuwa mwandishi wa
habari wa Gazeti la Mwanahalisi kama lingekuwa linaandika uchochezi mbona alikuwa
anaandika habari kwetu,harafu nataka niwaambieni huyu Nape ni source (Chanzo)
mzuri kwenye Gazeti letu hebu muulizeni.
Mpaka Fullhabari.blogs inaondoka polisi hapo Wahariri hao
walikuwa bado wapo kwenye Mahojiano
PICHA ZAIDI HIZO HAPO
Maoni 1
Tanzania hivi sasa chini ya utawala wa CCM wa awamu hii , hatutaiona tena harufu ya DEMOKRASIA na wala harufu ya FREEDOM of SPEECH .....na huko tunapoelekea is gonna be worse nabashiri hata wapinzani nao watakokotwa na kuwekwa vizuizini au kuuwawa ili CCM iendelee kwenye madaraka ..
Chapisha Maoni