KUMEKUCHA BONDE LA MKWAJUNI... WAKAZI WAFUNGA NJIA NA KUFANYA VURUGU
Hali
si salama hivi sasa katika eneo la Bonde la Mkwajuni Kinondoni jijini
Dar es salaam, na inaelezwa kuwa hali sio shwari kwani baadhi ya
Wananchi wamechoma mataili pande zote za barabara na hakuna gari kupita.
Jeshi la Polisi lipo eneo la tukio hivi sasa kukabiliana na tukio hilo
ambalo chanzo chake unadaiwa ni baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa
walikuwa wakazi wa eneo lililobomolewa ambao wameingia barabarani na
kufanya fujo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni