Zinazobamba

WAUZA MADAWA YA KULEVYA WAANZA KUPATA KIBANO,KAMANDA SIRRO,AWADAKA HAWA,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnjPOKkZCGVzHLzwYzzKoKu0KdxtS2waE4DoPqZcCFhyWONUIN96TAhWI2ihSnpkvbuSgh3iNQufFjH0PQnheK7YQ32_e_wDGMwVfY_fR91vj42Vo7u3KKNuRnQoC_ZNEWCdjuKUmNzxSn/s1600/IMG_1098.jpg
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Operasheni kali inayoendelea jijini Dar es Salaam


POLISI kanda Maalum ya Dar es Salaam imewashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa kuuza madawa ya kulevya hapa nchini huku wakiendelea kumuhoji mtuhumiwa mwingine kwa tuhuma hizo hizo.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

 Akizungumza  leo jijini hapa , Naibu kamishna wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Saimon Sirro, amesema watuhumiwa hao ni miongoni mwa wauza madawa wazoefu na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo(jana) kujibu mashakta yanayowakabiliwi.

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa na kilogramu 9 za madawa ya kulevya za aina ya heroine kutoka nchini Pakistan.
   Amewataja watuhumiwa hao sugu  wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuuza dawa  kulevya kamanda Sirro alisema ni pamoja,Mohamed Omari mkazi wa Tegeta nyuki (37) anayetuhumiwa kwa kusafirisha madawa ya kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu.

"Huyu mtu anatuhumiwa kwa kumsafirisha mtu ajulikanae kwa jina la Mwinyi Mgobanya mkazi wa ununio na kumuweka rehani huko Pakistan kisha akachukua madawa ya kulevya kwa mali kauli"

Akimtaja mtuhumiwa mwingine alisema ni Nassoro Suleiman ambaye ni meneja wa kampuni ya TUNGWE BUREAU De Change katika Jengo la IPS jijini hapa ambaye anatuhumuwa kwa kosa kwa kushirikiana na genge ka wauzaji wa madawa ya kulevya na kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha kwa njia ambazo zisizo rasmi.

Akizungumzia kuhusu mtuhimiwa ambaye anayeendelea kuhojiwa na jeshi la polisi, amtaja ni Daudi Adam miaka 46 mfanyabiashara mkazi wa salasala na kibaha.

"Huyu anatuhumiwa kusafirisha madawa ya kulevya lakini huyu atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi dhidi yake ukikamilika"

Akizungumzia kuhusu takwimu za mwaka2014 zinaonyesha kilogramu 304.91 za hereoni na kilogramu 68 za cocaine zilikamatwa na watuhumiwa 14501 ambapo miongoni mwao watanzania walikuwa 14467 ikilinganishwa na mwaka 2010 ambapo zilikamatwa kilogramu 123 za heroine.

Katika hatua nyingine kamanda Sirro alisema jeshi la polisi limefanikiwa kukamata magari 4 yaliyokuwa yameibwa maeneo tofauti ya jiji hili na mikoani.

Alimtaja John Samwel mkazi wa Mwanjelwa mkoani Mbeya alikamatwa kwa wizi wa gari aina ya Toyota IST, rangi nyeusi T 271 DCT iliyoibiwa nyumbani kwa Dr. Reginard huko Kimara.

Lingine ni fuso T 916 DCL aina ya Mitsbishi ambalo liliibwa maeneo ya kimara na kukutwa tegeta, gari lingine ni toyota Prado T593 CEL, lililoibiwa Regency Estate na gari aina prado DDB T999 iliyoibiwa maegesho ya Regency Estate iliyokamatwa huko Gezaulole.

Hakuna maoni