SAKATA LA KUFUKUZWA KAZI MLINZI WA LOWASSA LATINGA MIKONONI MWA MAGUFULI,BOSI TIS KITANZINI,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
Aliyekuwa mlinzi wa
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ofisa usalama mwandamizi, Aloyce
Tendewa, ambaye amefukuzwa kazi,
Sasa sakata la mlinzi huyo limefika mezani
kwa Rais John Magufuli na kumweka wakati mgumu Mkurugenzi mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa, Rashid Othuman.(Mtandao huu umetaarifiwa)
Tendewa ambaye alikuwa mlinzi wa lowassa
katika kipindi cha miaka kumi,alifukuzwa kazi juzi jioni na mwajiri wake ambaye ni Idara ya Usalama wa
Taifa (TIS) kwa kosa la kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kikazi.
Mbali na taarifa hizo, imeelezwa pia kuwa sababu nyingine ya
kufukuzwa kwake kazi kwa mwanausalama huyo ambayo hata hivyo haijathibitishwa,
ni madai ya kutoa taarifa za kubadilishiwa kituo chake cha kazi cha awali.
Taarifa za
kuaminika kutoka serikalini ambazo mtandao huu umepenyezewa zinasema sakata la
mlinzi huyo teyari limetinga kwenye ikulu ya Magufuli huku likimchukiza Rais na akataka
apewa taarifa kamili kuhusu mlinzi huyo,
Kinachotajwa
kumchukiza Rais Magufuli kuhusu hatua ya kufukuzwa Tendewa ,huku akiwa na historia yake ya ufanyaji kazi wake kwaa
uaminifu ndani ya serikali huku akishangaa kufukuzwa kwake kazi.
“Ndugu hili sakata sahivi limekuwa kuwa kubwa
sana,hata ajira ya mkurugenzi wa Usalama ipo pamoto sana,maana hili suala la
Tendewa limefika kwa Magufuli sahivi,tena Rais kachukia kweli maana mlinzi huyu
anahistoria ya kutukuka ndani ya nchi kwahiyo kufukuzwa kwake kazi kama mtu wa
aliyekuwa kibarua kumemchukiza Magufuli”akimesema Chanzo chetu hicho.
Sakata hili la Tendewa kufika kwa Rais Magufuli kuna
kuja ikiwa ni siku tatu kupita baada ya
vyombo vya habari nchini kuripoti juu ya kuondolewa kinyemela kwa mwanausalama
huyo kumlinda lowassa,
Tendewa alishirikiana na mwanausalama mwengine anaitwa
Samson Machaba ambao wote kwa pamoja ndio walikuwa walinzi wa Lowassa takribani
miaka kumi,ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya ofisi ya lowassa
zinasema kwa sasa lowassa ameachiwa mlinzi mmoja tu ambaye ni Samsoni Machaba
huku Tendewa akirudishwa serikali kabla ya kufukuzwa kazi kwake.
Kwa upande
mwingine taarifa zinaeleza kuwa mpango wa kutimuliwa kwa Tendewa uliandaliwa
kwa muda wa miezi kadhaa na barua ya kufukuzwa iliandikwa baada tu ya
kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.
Kwamba,
pamoja na sababu nyingine Tendewa anadaiwa kushindwa kuwasiliana inavyotakikana
na viongozi wake kuhusu majukumu yake ya kiulinzi wakati akiwa mlinzi wa
Lowassa.
Taarifa zinadai, kushindwa huko kwa Tendewa
kuliwafanya viongozi wake kufikia uamuzi wa kumfukuza kazi na kwamba barua yake
iliandikwa mapema Desemba mwaka jana, lakini hakukabidhiwa hadi hivi karibuni
alipovujisha siri za kuhamishwa kwake kituo cha kazi.
Mmoja wa watoa habari aliyeko serikalini ameeleza kuwa Tendewa aliundiwa kamati ya kumchunguza kuhusu kushindwa kutekeleza majukumu sawasawa ambayo ilifanya kazi kwa muda wa wiki mbili na kuwasilisha ripoti yake makao makuu.
Tendewa amefukuzwa kazi akiwa amebakiza mwaka mmoja
kustaafu utumishi wake katika Idara ya Usalama wa Taifa
UTATA
KUHUSU SAINI YA MTU ALIYEMFUKUZA KAZI.
Licha ya kupewa barua juzi jioni kutoka ndani ya (TIS)
hata hivyo barua ya kufukuzwa kazi Tendewa imeibuka utata juu ya nani aliyesaini
barua hiyo kwakuwa ingetakiwa kusainiwa na mkurugenzi mkuu lakini jambo la
ajabu imesainiwa na mtu wa chini.
HISTORIA YA TENDEWA.
Rekodi za utendaji kazi wa Tendewa zinaonyesha
kuwa baada tu ya kuajiriwa na TIS, alipelekwa katika kikosi cha walinzi wa
hayati Mwalimu Julius Nyerere na kutokana na uhodari wake aliaminiwa na
Mwalimu.


Aidha, rekodi hizo zinaonyesha kuwa Tendewa ni
miongoni mwa wana usalama wachache waliopigana vita ya kumng’oa aliyekuwa Rais
wa Uganda, Fashisti Iddi Amini Dada mwaka 1978 na 1979 na akiwa vitani alitekwa
na kwenda kuzuiliwa nchini Sudan.
Historia
hiyo inaonyesha kuwa Tendewa aliokoka kuuawa kwa risasi akiwa mateka muda mfupi
baada ya kurejeshwa nchini kutoka Sudan siku chache baada ya Rais Yoweri
Museveni kushika madaraka ambapo mmoja wa walinzi wanawake wa rais alimuona na
kumtambua kuwa alikuwa mmoja wa wapiganaji hodari wa Tanzania na si muasi kama
ilivyokuwa ikidhaniwa hivyo alirudishwa Tanzania.
Baada ya
kurejeshwa nyumbani alipewa jukumu la kuwa mlinzi wa Mwalimu Nyerere na hata
alipong’atuka madarakani aliendelea na kazi hiyo hadi Mwalimu alipofariki dunia
katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas London nchini Uingereza
Maoni 1
HIVI TUNAELEKEA WAPI KWA KUWAFANYIA MASHUJAA WA NCHI YETU HIVI??...TUNATEGEMEA KUZALISHA MASHUJAA WA AINA GANI HAPO BAADAE?
Chapisha Maoni