Zinazobamba

RUNGU LA MAGUFULI LAHAMIA KWA BODABODA.MRITHI WA KAMANDA KOVA DAR,AWATANGAZIA KIAMA,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnjPOKkZCGVzHLzwYzzKoKu0KdxtS2waE4DoPqZcCFhyWONUIN96TAhWI2ihSnpkvbuSgh3iNQufFjH0PQnheK7YQ32_e_wDGMwVfY_fR91vj42Vo7u3KKNuRnQoC_ZNEWCdjuKUmNzxSn/s1600/IMG_1098.jpg
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Operasheni kali inayoendelea jijini Dar es Salaam

NA KAROLI VINSENT
JESHI  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam,limetangaza opareshini  kabambe ya kuzikagua  pikipiki zote aina ya (Bodaboda) kuangalia usajili wake,
Pamoja na kuweka ulinzi mzito ili kuhakikisha zisingie katika kati ya Jijini .
 Akitangaza oparesheni hiyo,Kamanda wa polisi wa Kanda Maluum ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo,
Kamanda Sirro amesema baada ya jeshi hilo kubaini kuwa vitendo vingi vya ujambazi vimekuwa vikifanywa na waendesha Pikipikia hao,basi wameamua kufanya msako mkali ikiwemo kuzikagua piki piki hizo ili kuziangalia uhalari wake,
Amesema katika Oparesheni hiyo wamefanikiwa kuzikamata pikipiki hizo katika maeneo tofauti,
Ameyataja maeneo hayo ni Wilaya ya Temeke ambapo wamefakiwa kuzikamata pikipiki 130 ambapo kati ya hizo 55 zimelipiwa fainiiiiiiiiiii na pikipiki 75 zinashikiliwa Vituoni kwa uchunguzi.
Sehemu nyengine ni Wilaya ya Ilala wamefanikiwa kuzikamata pikipiki 249,ambapo pikipiki 90 zimetozwa faini huku pikipiki 10 zimeachiwa huru na 95 zikiwa zimeshikiliwa vituoni kwa uchunguzi.
Mbali na Ilala,sehemu nyengine ni wilaya ya Kinondoni ambapo wamefanikiwa kuzikamata pikipiki 241 ambapo kati ya hizo 90 zimetozwa faini pikipiki 10 zimelipiwa faini,pikipiki 19 zimeachiwa huru na pikipiki 95zinashikiliwa kwa uchunguzi,
Hata hivyo Kamanda Sirro amesema kwa sasa Jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linazikamata pikipiki zote ambazo zimekaidi katazo lilowakataza kuingia mjini,
Katika hatua nyengine Jeshi hilo pia limewataka WAMILIKI wa Taasisi za Kifedha kutakiwa kujiridhisha kama waajiliwa katika taasisi hizo kama wanahusika kwa njia moja ama nyingine katika uharifu unaohatarisha maisha ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam,  
Kamanda Sirro amesema kuwa hatua za makusudi zimechukuliwa katika maeneo mbalimbali hasa ya eneo la Kibiashara la Mlimani City kutokana na matukio mengi ya uporaji  wa fedha kwa kutumia pikipiki.
  Pia amesema kuwa pamoja na sheria hizo kuchukuliwa watafanya operasheni maalumu katika eneo hilo na kutafuta namna nzuri ya kuondoa pikipiki katika maeneo hayo.
   Katika Operasheni zilizofanywa na Jeshi hilo wamefanikiwa kuwakamata majambazi nane pamoja na kumamata Bunduki mbili aina ya Pump Action ambazo namba zake zilifutwa na kukatwa Mtutu.
   Aidha Kamanda Sirro amesema kuwa katika Operasheni hiyo wamemkamata jambazi aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kama Mkama Hassan mkazi wa Gomgolamboto jijini Dar es Salaam na alipopekuliwa alikutwa na Bastola aina ya Chinese iliyofutwa namba ikiwa na magazine yenye risasi saba. 

 


Hakuna maoni