MAALIM SEIF AISHIKA MOYO WA ZANZIBAR,KWANI ANAWEZA KUAMUA CHOCHOTE,SOMA HAPO KUJUA
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF),
Maalim Seif Shariff Hamad ndiye aliyeshika amani ya visiwa vya Zanzibar. Anaandika Faki Sosi …
(endelea).
Utulivu wake katika kukabiliana
na dhuluma inayotaka kutendwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar
ndiko kunakovifanya visiwa hivyo kuwa salama.
Bila
shaka, Maalim Seif ikifika mahali akisema ‘liwalo na liwe’ Zanzibar itazama
kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hali ya siasa Zanzibar si shwari, wananchi
wanaweweseka kutokana na kutokujua kesho yake itakuwaje.
Hatua
ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta
matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana ndiyo iliyoitumbukiza
Zanzibar kwenye mashaka.
Hotuba
ya Maalim Seif aliyoitoa juzi jijini Dar es Salaam, inaashiria uvumilivu
uliotukuka lakini pia inabeba ujumbe wa kuelekea kuchoka. Si vyema kupuuza
hilo.
CCM
inagoma kuondoka madarakani, inafanya juhudi kuhakikisha inaendelea kushika
hatamu licha ya kukataliwa na Wazanzibari.
Ukweli
ulio wazi, Maalimu Seif ametumia nguvu kubwa kuwatuliza wananchi visiwani humo
ili kulinda amani na utulivu wa visiwani uliopo sasa.
Kauli
ya Maalim Seif kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu, inaweza kutafsirika vibaya
na makada wa CCM, kauli hiyo haiashirii unyonge hata kidogo.
Maalim
Seif wakati mwingine ndivyo alivyo, wakati mwingine huonesha tabasimu hata kama
pale jambo analozingumzia kuwa zito.
Namna
ilivyo, Wazanzibari wamechoka, subira yao ipo mikononi mwa Maalim Seif,
wamechoka kwa sababu wamechoshwa. Hawa wanasubiri kipenga kipulizwe.
Kauli
ya Dk. Ali Mohammed Shein ambaye anaendelea mkung’ang’ania madaraka kwamba
uchaguzi utarudiwa, inaashiria shari.
Amekiri
mbele ya umma kwamba majadiliano yanaendelea lakini hapo hapo anatoa hitimisho
kwamba, uchaguzi utarudiwa, Dk. Shein anatangaza ubabe kwamba iwe iwavyo
uchaguzi utarudiwa.
Dk.
Shein anatangaza uchaguzi kurudiwa huku nyuma ya mgongo wake Jecha akipokea
amri. Tafsiri inayochomoka hapa ni kuwa kauli ya Dk. Shein ndio kauli ya Jecha.
Ni
vema Dk. Shein akaijali Zanzibar, akathamini uamuzi wa wananchi wake kwamba,
zama za CCM zimefika tamati. Kinyume cha hivyo ni umwagaji damu jambo ambalo
halipendezi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni