Zinazobamba

KAMNDA SIRRO AZIDI WAKAMATA WAUZA MADAWA YA KULEVYA,SOMA HAPO KUJUA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnjPOKkZCGVzHLzwYzzKoKu0KdxtS2waE4DoPqZcCFhyWONUIN96TAhWI2ihSnpkvbuSgh3iNQufFjH0PQnheK7YQ32_e_wDGMwVfY_fR91vj42Vo7u3KKNuRnQoC_ZNEWCdjuKUmNzxSn/s1600/IMG_1098.jpg
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na madawa yadhaniwayo ni ya kulevya yenye uzito unaofikia kilo moja.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dare s Salaam,Kamanda wa Kanda hiyo,Naibu kamishna wa Polisi,Saimon sirro amesema watuhumiwa  hao walikamatwa tarehe 27/1/2016 maneno ya kinondoni ufipa majira ya saa tano asubuhi baada ya kikosi kazi cha kupambana na madawa ya kulevya kupokea taarifa  kutoka kwa raia mwema.
Sirro amesema Jeshi hilo baada ya kupata taarifa hizo wakaweka mtego na uliofanikisha kukamatwa watuhumiwa hao kwenye gari namba 7984 cgz aina ya Toyota IST,
Hata hivyo sirro hakuyataja majina ya watuhumiwa hao kwa sasa kwasababu ya kiupelelezi,ambapo Unga huo unaliokamatawa umepelekwa kwenye ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi,
Katika hatua nyengine Jeshi hilo la polisi limefanikiwa kuwakamata watu watatu kwa tuhumza za kukutwa na nyara za serikali  ambazo ni meno ya matano ya Tembo,
Sirro amesema watuhimiwa hao walikamatwa ,namo tarehe 22/01/2016  majaira ya usiku huko Kibamba Hospotali kata ya kibamba wilaya ya kimara,Kinondoni jijini hapa ,
Ambapo amedai polisi walipokea taarifa kuwa kuna mfanyabiashara anauza nyara hizo,jambo lilowafanya Polisi kuweka mtego na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa hao,
Watuhumiwa hao ni Ibrahimu Samwel,mkazi Temeke jijini hapa,Amriiiis Francis,miaka 44,mkazi wa Tanga, pamoja na Jailan Mohamed,miaka 33,mkazi wa Magomeni jijini hapa

Hakuna maoni