CCM YAENDELEZA UBABE WAKE UCHAGUZI WA UMEYA JIJINI DAR,WAJA NA KITUKO HIKI,MBUNGE KUBENEA NAYE AAPA KUFIA MAHAKAMANI KUTAFUTA HAKI,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea akitoa hoja katika mkutano wa uchaguzi wa Meya katika Manispaa ya Kinondoni |
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetia mpira kwapani kwa
kukimbilia mahakamani baada ya kuona mazingira ya kushinda Ilala na Kinondoni
hayawezekani kwa namna yeyote. Anaandika Sarafina Lidwino ….
(endelea).
Zoezi la uchaguzi ambalo
lilipaswa kwenda sambamba na uapishwaji wa Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni na
Ilala umeahirishwa kwa zuio la Mahakama ya Kisutu.
Akisoma
zuio hilo Mwanasheria wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Burton Mahenge
amesema amepokea zuio hilo leo asubuhi lililojumuisha Manispaa zote mbili za
Kinondoni na Ilala. Ingawa baada ya kuongea na waandishi wa habari hawakueleza
imekuwaje Mahakama ikatoa zuio siku ya Jumamosi, tena mahakama ya Kisutu
kupinga amri iliyotolewa na mahakama kuu ijumaa kwa kesi hiyo hiyo kuhusu
uchaguzi wa manispaa hizo.
Mahenge
amesema zuio hilo lenye jarada la MISC Civil Application Na 7 ya mwaka 2016 na
kupewa kesi ya madai ya msingi Na. 1 ya mwaka 2016 haikueleza sababu za zuio
hilo kwa kuwa imesikilizwa upande mmoja.
Akizungumza
na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo amesema, kesi hiyo ya madai
imefunguliwa na Elias Phiremon Nawera mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
akiitaka mahakama kusitisha uchaguzi wa Ilala na Kinondoni.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Aron Kagurumjuli
mara baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo amesema,
“Agizo
la mahakama niliipokea jana saa 12 jioni, hivyo nikashindwa kuwajulisha wajumbe
kuwa hakutakuwa na mkutano kutokana na muda. Sina budi kutii amri ya mahakama
kwani ningeendeleza mjadala ningekiuka sheria”.
Alipoulizwa
ilikuwaje akapokea zuio hilo usiku saa 12:00 na wakati haukuwa muda wa kazi,
alisema yeye huwa anafanya kazi usiku na mchana, ana muda wa kuingia ofisini
hana muda wa kutoka.
Aidha
amesema, zuio hilo la mahakama lilitolewa jana na kupelekwa ofisi kwake jioni.
Hivyo kesi hiyo itasikilizwa January 13 mwaka huu mahakamani hapo.
“Mimi
siwezi kuhoji sana kwanini Mahakama kuu iliruhusu shughuli hii ifanyike leo
halafu mahakama ndogo ya Kisutu leo imetoa zuio, mimi natii agizo la mahakama
hadi pale itakapo sikiliza kesi hiyo na kutoa uamuzi”, amesema Kagurumjuli.
Uchunguzi
uliofanywa na mwanahalisi online, umebaini kuwa vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) nao tayari walishaleta wabunge wa viti maalumu
kutoka Zanzibar na Pemba ili kuikabili vema CCM iliyoleta wabunge kutoka
Zanzibar kwa ajili ya kupiga kura Kinondoni. Hadi jana asubuhi Ukawa walikuwa
na madiwani 44 dhidi ya CCM iliyokuwa na 31 katika uchaguzi huo.
CCM
iliingia pamoja na Mawaziri wawili, Makame Mbarawa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Pamoja na Augustine Mahiga Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa
kikanda na kimataifa ambao kwenye kikao cha awali kilichoahirishwa hawakuwepo.
Wakati
huo huo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Saed Kubenea Amesema kuwa, wamesikitishwa sana na
kilichotokea leo kwani hawakutarajia.
Kubenea
amesema, wanatarajia kwenda mahakamani siku hiyo ya kusomwa kesi na kusikia
sababu za kesi hiyo kufunguliwa. “ Tunauhakika mtu aliyefungua kesi hiyo hana
mamlaka iwaje mwananchama wa kawaida afungue kesi tena asiyekuwa mkazi wa
kinondoni?”.
“Baraza
la Madiwani kinondoni halipo tangu mwezi wa saba mwaka jana je wananchi
wataishi vipi bila uongozi wa chini? tunawasiwasi na mahakama zetu kujihusisha
na mambo ya kisiasa. Sisi hatutakubali tutafuatilia hadi tupate haki yetu kwani
ushindi ni wetu,” amesema Kubenea
Hakuna maoni
Chapisha Maoni